Jumamosi ya Januari 27, 2018 kutakuwa na mechi ya VPL kati ya Azam FC dhidi ya Yanga mechi hii inatolewa sana macho kuanzia na timu zenyewe lakini pia mashabiki na wadau wa soka macho yao yatakuwa kwenye game hii.
Kuelekea mechi hiyo, Azam wameshatuma barua kwa kamati ya waamuzi wakimkataa mwamuzi wa kati Israel Mujuni Nkongo ambaye amepangwa kucheza mechi hiyo.
Abdukarim Nurdin ni makamu mwenyekiti wa klabu ya Azam ametaja hoja zao za kumkataa Nkongo asichezeshe mechi hiyo inayovikutanisha vilabu vyenye majina makubwa kwenye ligi kuu.
“Kumkataa mwamuzi sio dhambi tumepeleka maombi yetu kwa hiyo wao wenyewe ndiyo wenye maamuzi watubadilishie au wamwache huyohuyo, lakini hii mechi inachezwa Dar kwa nini mwamuzi atoke hapaha Dar?
“Ukiangalia mechi zetu nyingi ambazo anachezresha yeye zinakuwa na utata lakini juzi tu katoka kuvuruga mechi ya Mbeya City na Prisons na watu wote wameona kwa hiyo sisi tumepeleka ombi linaweza kukubaliwa au kukataliwa. Tupo nyumbani na kesho tunatarajia ushindi tuweze kupata pointi tatu.”
Azam ipo katika nafasi ya pili kwenye msimamo wa ligi ikiwa na pointi 30 baada ya kucheza mechi 14, ipo nyuma ya vinara wa ligi Simba kwa pointi mbili, Yanga yenyewe ipo nafasi ya tatu kwa pointi zake 25. Timu zote zinatafuta pointi tatu ili kuendelea kukimbizana kwenye mbio za ubingwa wa msimu huu 2017/18.
No comments:
Post a Comment