Waziri
wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Harrison Mwakyembe
akizungumza alipokutana na wadau wa sekta anazozisimamia kuhamasisha
wadau hao kuunga mkono kampeni ya uzalendo itakayozinduliwa na Rais wa
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli tarehe
nane Desemba Mkoani Dodoma leo Jijini Dar es Salaam.
Naibu
Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Juliana Shonza
akizungumza wakati Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe.
Harrison Mwakyembe alipokutana na wadau wa sekta anazozisimamia
kuhamasisha wadau hao kuunga mkono kampeni ya uzalendo itakayozinduliwa
na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli
tarehe nane Desemba Mkoani Dodoma.
Kaimu
Mkurugenzi Idara ya Maendeleo ya Sanaa Bibi. Leah Kihimbi (wapili
kushoto) akizungumza wakati Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo
Mhe. Harrison Mwakyembe (wapili kulia) alipokutana na wadau wa sekta
anazozisimamia kuhamasisha wadau hao kuunga mkono kampeni ya uzalendo
itakayozinduliwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt.
John Pombe Magufuli tarehe nane Desemba Mkoani Dodoma. Kushoto ni Naibu
Waziri wa Habari Mhe. Juliana
Mjumbe
wa kamati ya uzalendo Bw. Mrisho Mpoto (kulia) akizungumza wakati
Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Harrison Mwakyembe
(katikati waliokaa) alipokutana na wadau wa sekta anazozisimamia
kuhamasisha wadau hao kuunga mkono kampeni ya uzalendo itakayozinduliwa
na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli
tarehe nane Desemba Mkoani Dodoma. Wapili kushoto ni Naibu Waziri wa
Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Juliana Shonza
Mwanamziki
mkongwe nchini Bw. John Kitime (aliyesimama) akichangia wakati Waziri
wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Harrison Mwakyembe (hayupo
pichani) alipokutana na wadau wa sekta anazozisimamia kuhamasisha wadau
hao kuunga mkono kampeni ya uzalendo itakayozinduliwa na Rais wa Jamhuri
ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli tarehe nane
Desemba Mkoani Dodoma.
Baadhi
ya wadau wa sekta za Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo wakifuatilia
matukio mbalimbali yaliyokua yakiendelea wakati Waziri wa Habari
Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Harrison Mwakyembe (hayupo pichani)
alipokutana na wadau wa sekta anazozisimamia kuhamasisha wadau hao
kuunga mkono kampeni ya uzalendo itakayozinduliwa na Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli tarehe nane Desemba
Mkoani Dodoma.
Naibu
Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Juliana Shonza
(kushoto) akimkabidhi mshindi wa shindano la Ubingwa wa Dunia uzito wa
kati Bw. Ibrahim Class hundi ya shilingi milioni kumi na nane wakati
Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Harrison Mwakyembe
(hayupo pichani) alipokutana na wadau wa sekta anazozisimamia
kuhamasisha wadau hao kuunga mkono kampeni ya uzalendo itakayozinduliwa
na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli
tarehe nane Desemba Mkoani Dodoma.
Picha na: Genofeva Matemu – WHUSM
Waziri
wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Dkt Harrison Mwakyembe
amewataka Watanzania wote kujitokeza katika Uzinduzi wa Kampeni ya
kitaifa ya Uzalendo inayotarajiwa kuzinduliwa tarehe 08 Desemba 2017
mjini Dodoma na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt John
Pombe Magufuli.
Akizungumza
na Waandishi wa Habari leo Jijini Dar es Salaam Mhe. Mwakyembe amesema
kuwa Wizara yake imeamua kuanzisha Kampeni ya Uzalendo ili kuwakumbusha
watanzania kupenda,kujali na kuthamini nchi yao kwa kuenzi na kuupenda
Utamaduni wa Taifa letu ambao ndio unaounganisha na kutambulisha
watanzania.
“Uzalendo
wetu umetikisika ni lazima sasa kuamka na kujua kuwa tuna jukumu la
kuenzi Uzalendo tuliojengewa na Waasisi wa Taifa letu wa kupenda nchi
yetu na kudumisha Utamaduni wetu”Alisema Mhe. Waziri Mwakyembe.
Aidha
amewataka watanzania pia kutumia lugha ya Kiswahili kwa ufasaha katika
maisha ya kila siku kwa kuwa Lugha hiyo ndio inayotambulisha Mtanzania
popote anapokuwa pamoja na kuheshimu alama zote za Taifa ikiwemo Bendera
ambapo ameagiza matumizi sahihi ya Bendera hiyo.
Kwa
upande wake Naibu Waziri wa Wizara hiyo Mhe. Juliana Shonza amesema
Kampeni hiyo ni muhimu sana kwa Taifa letu kwakua inalenga kukumbusha
jamii Utamaduni wetu ambao ndio unafanya jamii kuwa na uzalendo katika
nyanja zote za maendeleo.
“Ili
kufikia adhma ya Serikali ya awamu ya Tano ya Tanzania ya Viwanda bila
kuwa na uzalendo wa kufanya kazi kwa bidii na kwa kushirikiana.” Alisema
Mhe. Juliana.
Mhe.
Juliana ameongeza kuwa Wasanii wanahabari na wanamichezo wanajukumu
kubwa sana la kuutangaza Kampeni hii lakini pia kuelimisha jamii maana
ya Uzalendo pamoja na kuwa mstari wa mbele katika kutenda mambo mazuri
yanayoendana na Utamaduni wa Tanzania kwa wao ni kioo cha jamii.
Naye
msanii Mrisho Mpoto ameiahidi Serikali kushirikiana nayo katika
kuelimisha jamii maana ya uzalendo kupitia sanaa yake ambapo amesema
atashirikiana na wasanii wenzake kuandaa nyimbo zitakazowakumbusha
watanzania umuhimu wa Uzalendo ili kuwa na Taifa lenye jamii inayotambua
maana ya uzalendo kama ilivyokuwa enzi za mababu zetu.
Kampeni
ya uzalendo yenye Kauli mbiu “UZALENDO NA UTAIFA,NCHI YANGU KWANZA” ina
lengo la kurejesha hali ya watu kupenda nchi yao kupinga mmomonyoko wa
maadili kwa viongozi wa Umma,kuongezeka kwa tuhuma za rushwa,kuibuka
kwa ufisadi,matumizi mabaya ya mamlaka na ubaguzi wa aina yeyote ambapo
itakuwa inaadhimishwa kila mwaka.
No comments:
Post a Comment