Mkurugenzi wa Taasisi
inayotoa mikopo kwa mabenki na Taasisi nyingine za kifedha kwaajili ya Ujenzi
na ununuzi wa nyumba (TMRC),Oscar Mgaya akikabidhi mfano wa hundi yenye dhamani ya
shilingi milioni nane kwa Kaimu Mkurugenzi wa
Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (JKCI), Profesa Mohamed Janabi, kwaajili ya matibabu ya moyo kwa watoto wane (4)
ambao wamekosa pesa kwaajili ya matibabu hayo kushoto ni Mkurugenza wa Fedha wa
TMRC, Oswald Urassa. Na wengine ni maofisa wa hospitali hiyo
makabidhiano hayo yamefanyika jana jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi wa Taasisi inayotoa Mikopo kwa Mabenki na Taasisi nyingine za kifedha
kwaajili ya Ujenzi na ununuzi wa nyumba (TMRC),Oscar Mgaya wapili ( kushoto) akifafanua jambo wakati wa hafla ya
kukabidhi msaada wa shilingi milioni nane kwaajili
ya matibabu ya moyo kwa watoto wanne (4) ambao hawana uwezo wakupata pesa
kwaajili ya matibabu hayo
TAARIFA
KWA VYOMBO VYA HABARI
TMRC
YAWEZESHA UPASUAJI WA MOYO KWA WATOTO WANNE
14, DESEMBA 2017 - (DAR
ES SALAAM), Kampuni ya Tanzania Mortgage
Refinance Limited (TMRC), imetoa msaada wa kiasi cha Shilingi milioni Nane
(Shilingi 8,000,000) kwa ajili ya upasuaji
wa moyo kwa watoto wanne jijini Dar es Salaam.
Akikabidhi
mfano wa hundi hiyo ya Shilingi milioni Nane kwa Kaimu Mkurugenzi wa Hospitali
ya Taifa ya Muhimbili (JKCI), Profesa Mohamed Janabi, Afisa Mtendaji Mkuu (CEO)
wa TMRC, Oscar Mgaya, alisema kuwa wameamua Kuitikia wito huu wa kuwasaidia
watoto hao ambao hawana uwezo na bila msaada huo pengine wasingeweza kupata
huduma hiyo na maisha yao yangekua hatarini.
"Tumeamua
kusaidia tiba kwa hawa watoto baada ya kuona tangazo kwenye kituo cha
televisheni cha Clouds. Hivyo basi, tukaona umuhimu wa kufanikisha malipo kwa
ajili ya upasuaji wa watoto hawa wanne," Bw. Mgaya alisema.
Aidha,
Mtendaji Mkuu huyo, alisema taasisi yake hiyo ambayo inatoa mikopo ya ujenzi au
ununuzi wa nyumba kupitia mabenki na taasisi nyingine za fedha kuwa, waliamua
kutoa kiasi cha Shilingi milioni mbili (Shilingi 2,000,000) kwa upasuaji wa
kila mtoto kwa kuwa ni taifa la kesho.
Hii ni sehemu ya kutekeleza wajibu wetu katika jamii (corporate social
responsibility).
"Tumeamua
kutoa kiasi kidogo kwa watoto hawa
wadogo ambao miongoni mwao wana ndoto za kuwa wataalamu wa benki, madaktari, marubani
n.k. Hivyo, taasisi yetu imeona umuhimu wa kufanya ndoto za hawa watoto kutimia
kwa kuwawezesha kupata tiba," alisema.
Bw.
Mgaya ametoa rai kwa wadau wengine kujitokeza kusaidia wenye uhitaji wa tiba
hii ya moyo hasa kwa wale wenye maisha duni ambapo uhitaji unaelezewa kuwa ni
mkubwa.
Kwa
upande wake, Kaimu Mkurugenzi wa Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (JKCI),
Profesa Mohamed Janabi, alisema kwamba taasis yake imejipanga kuhakikisha kuwa
inaendelea kupunguza idadi ya wagonjwa wanaoenda kutibiwa nje ya nchi, kutokana
na magonjwa ya moyo na badala yake kutibiwa nchini kwa gharama nafuu.
"Licha
ya kuwasaidia watanzania kupunguza gharama kwa matibabu ya moyo hapa nchini
badala ya nje ya nchi, pia hii imepunguza sana gharama ambazo serikali imekuwa
ikizitumia kila mwaka kutibu maradhi kama hayo nje ya nchi," Prof Janabi
alisema.
Tangu taasisi yetu ianze kutoa tiba hii mwaka 2008, tumeweza
kupunguza kwa kiwango kikubwa idadi ya watanzania wanaotibiwa nje ya nchi. Hata
hivyo, ameishukuru TMRC, kwa msaada wa fedha kwa ajili ya tiba kwa watoto hao
wanne na kuziomba taasisi nyingine kuiga mfano.
“Taasisi yetu inahamasisha watu kuchangia milioni 2 kwa ajili
ya watoto walio katika hali ngumu na kiasi kingine kinachangiwa
na serikali. Kwa wiki hii tumejipanga kufanya upasuaji kwa watoto 60 na hii ndiyo zawadi ya Sikukuu ya Krismas
toka kwetu,” alisema Prof. Janabi.
Hadi sasa, Prof. Janabi alisema kuwa watoto 300
wameshafanyiwa upasuaji wa moyo toka Januari hadi sasa ingawa lengo ilikuwa ni
kufikia watototo 400.
Akizungumzia kuhusu uhitaji wa huduma hii ya upasuaji wa
moyo, Prof. Janabi alisema kuwa ni mkubwa sana ambapo kati ya watoto miloini 2
wanaozaliwa, asilimia 1 wanatatizo la moyo.
“Miongoni
mwa mambo yanayosababisha tatizo la moyo kwa watoto linatokana na wazazi
kutozingatia chanjo, lishe nakadhalika,” alisema
No comments:
Post a Comment