Mwakilishi wa QNET
Tanzania, Benjamin Mariki akikabidhi misaada mbalimbali ikiwepo vyakula na
mahitaji muhimu ya kibinadamu kwa mlezi wa kituo cha kulelea watoto yatima
cha Khayraat Orphans Centre kilichopo Kigogo Kati, Bi. Khadija Hussein hafla ya
makabidhiano hayo imefanyika katika kituo hicho jijini Dar es Salaam leo wengine pichani ni baadhi ya watoto wanaolelewa katika kituo hicho.
Mwakilishi wa QNET Tanzania, Benjamin Mariki (kulia) akikabidhi
mashine ya kusafishia maji ya kunywa (water purifier) pamoja na
mahitaji mengine ya kibinadamu kwa mlezi
wa kituo cha kulelea watoto yatima cha Khayraat Orphans Centre kilichopo
Kigogo Kati, Bi. Khadija Hussein, hafla ya makabidhiano hayo imefanyika katika
kituo hicho jijini Dar es Salaam leo.

QNET
imetoa Msaada wa mashine ya kusafishia maji (water purifier) na vyakula kwa
watoto yatima wa kituo cha Khayraat, Dar es salaam
Tarehe
20th Desemba, Dar es salaam – Moja kati ya
taasisi inayokua kwa kasi sana Tanzania ya masoko ya mtandao QNET, leo imetoa
msaada wa mashine yenye mfumo wa kusafisha maji ya Water purifier na chakula
chenye thamani ya zaidi ya Tsh milioni 2 kwa kituo cha watoto yatima cha
Khayraat jijini Dar es salaam.
Msaada wa QNET ni
sehemu ya juhudi za kampuni hiyo za kuwajibika katika jamii, ambazo zimeelekezwa
katika kutoa msaada wa upatikanaji wa maji safi na salama kwa zaidi ya watoto
500 wenye uhitaji katika kituo cha kulelea watoto yatima na kuwapatia chakula kwaajili
ya kuwawezesha kufurahia sikukuu za krimasi katika kipindi hiki cha sikukuu
kama watoto wengine.
Kwa mujibu wa
mwakilishi wa QNET Tanzania Benjamin Mariki, kampuni ya mauzo ya moja kwa moja ina
sera bora ya uwajibikaji kwa jamii ambayo inatafuta kutoa kwa jamii inayoihudumia.
“Katika kampuni ya
QNET, tunaamini kuwa zaidi ya kusambaza bidhaa zenye ubora wa kiwango cha juu
kwa wateja wetu, tuna jukumu la kusaidia serikali na wadau wengine katika
kutekeleza shughuli ambazo zina athari nzuri kwa jamii, hasa miongoni mwa
wanajamii wenye uwezo mdogo,” alisema Mariki.
Mariki alisema kuwa
msaada uliotolewa kwaajili ya kituo ni pamoja na ufungaji wa mashine ya
kusafishia maji, kilo 100 za Mchele, kilo 100 za maharage, kilo 100 za unga,
lita 60 za mafuta ya kupikia, kilo 100 za sukari, kilo 100 za sabuni ya kufulia
pamoja na biskuti, pipi na juisi.
Akipokea msaada huo,
Mwasisi wa kituo cha Khayraat Orphans Centre, Bi Khadija Khussein aliishukuru
kampuni ya QNET kwa kutoa msaada akisema kuwa msaada huo utawasaidia kwa
kiwango kikubwa watoto walioko kituoni.
“Tunashukuru kwa msaada
huo tukiwa tunatambua kuwa mashine ya kusafishia maji ya water purifier
itasaidia katika kurahisisha upatikanaji wa maji safi na salama kwaajili ya
watoto, hivyo kutoa uhakika wa afya kwa watoto kwa kuzuia magonjwa yanayoambukizwa
kwa maji kama vile typhoid na Kipindupindu wakati vyakula vitawapa watoto nafasi
ya kufurahia sikukuu ya krimasi na mwaka mpya”. Alibainisha Bi Khussein
Kuhusu QNET
Ni kampuni maarufu ya
mauzo ya moja kwa moja yenye asili ya Asia, QNET inatoa aina mbalimbali za
bidhaa za kuboresha maisha ambazo zinatolewa kupitia mfumo wake wa biashara ya
mtandao (e-commerce) kwa wateja na wasambazaji katika zaidi ya nchi 100.
Kampuni hii pia ina baadhi ya ofisi zake na Mawakala katika nchi 25 duniani
kote, na zaidi ya watayarishaji 50, nje ya waendeshaji wa ndani ya nchi au mawakala
katika nchi kadhaa.
QNET ni mwanachama wa
Chama cha wauzaji wa moja kwa moja (Direct Selling Association) cha Malayasia,
Singapore, Ufilipino na Indonesia. QNET pia ni sehemu ya Chama cha Chakula Bora
cha Hong Kong (Hong Kong Health Food Association) na Chama cha viwanda vya
Virutubisho vya afya cha Singapore (Health Supplements Industry Association)
miongoni wa vingine.
QNET pia inafanya vizuri katika kudhamini michezo dunia kote,
ikijumuisha mpira wa miguu (Mshirika wa moja kwa moja wa mauzo wa Klabu ya Manchester
City), Mashindano ya Magari ya fomula One, badminton na zaidi, kufuatia imani
thabiti ya kampuni ya QNET kwamba msukumo, ari na kufanya kazi kwa pamoja
katika michezo kunaendana na ule wa QNET
Kwa maelezo zaidi
kuhusu QNET, Tafadhali tembelea Wavuti ya QNET, www.qnet.net
No comments:
Post a Comment