Katika
kuunga Mkono juhudi zinazofanywa na Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaamPaul
Makonda kusaidia Watu wenye uhitaji wa miguu bandia na zoezi la upimaji
afya,Kampuni ya China Nationali building Material Group leo imekabidhi
hundi ya Shilingi Milioni kumi.
Akizungumza
na Waandishi wa habari mara baada ya kupokea msaada huo kwa niaba ya
Mkuu wa Mkoa Mganga Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Dakta Grace Magembe
amesema Serikali ya Mkoa imekusudia kutatua changamoto za kiafya kwa
wananchi pamoja na kusaida watu wenye ulemavu,ambapo amebainisha kuwa
hapo awali Serikali ya Mkoa ilikusudia kusaidia watu wenye ulemavu
miambili lakini idadi ya wenye uhitaji wa miguu ni zaidi ya watu elfu
moja hivyo amewataka wadau kuendelea kujitokeza kusaidia.
Dakta
Magembe ameongeza kuwa tokea kuingia madarakani Serikali ya awamu ya
tano ilio chini ya Rais Dakta John Magufuli imekuwa ikishughulikia
changamoto mbalimbali za wananchi hivyo amewataka wananchi kuendelea
kuunga mkono juhudi hizo.
Kwa
upande wake Kaimu Meneja Mkuu wa Kampuni ya China National building
Material Group Wang Shupeng amesema kampuni hiyo imeridhishwa na juhudi
zinazofanywa na Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam na imetambua umuhimu wa
kusaidia watu wenye mahitaji maalumu ikiwemo miguu bandia hivyo mbali na
msaada huo wa shilingi milioni kumi za kitanzania itaendelea kutoa
misaada mbalimbali kwa Serikali.
Picha ya pamoja
No comments:
Post a Comment