A great place to access the latest news and information.

Breaking

Post Top Ad

Your Ad Spot

Friday, November 10, 2017

VIONGOZI WOTE WALIOHUSIKA KUPOKEA MIFUGO PAMOJA NA WAFUGAJI KUTOKA NJE YA NCHI WACHUKULIWE HATUA ZA KISHERIA-WAZIRI MPINA

WAZIRI wa Mifugo na Uvuvi Luhaga Mpina, ameagiza Viongozi wote waliohusika kupokea mifugo Pamoja na wafugaji kutoka Nje ya nchi kuchukuliwa hatua za kisheria  baada ya uchunguzi kukamilika, ikiwa ni pamoja na kuwafukuza kazi baadhi ya watendaji watakao gundulika walijihusisha na suala hilo ambalo ni kinyume na maadili ya utumishi wa umma.

Hata hivyo Waziri huyo alisema kuwa zoezi la ukamataji wa Ng'ombe zilizo ingizwa nchini kinyume na utaratibu, jumla yake ni Ng'ombe 1580 ambao wanashikiliwa, na akaagiza kuwa Ng'ombe hizo zitaifishwe na kupigwa mnada baada ya uchunguzi kukamilika na kuhakikisha ifikapo Novemba 10 mwaka huu Mifugo yote iliyoingia kinyume na utaratibu iwe zimeondolewa kabisa.

Akizungumza juzi mara baada ya ukamataji wa Ng'ombe Wilayani kasulu Mkoani Kigoma, Mpina alisema viongozi walioshiriki kupokea mifugo kutoka Nje ya Nchi,  viongozi wa aina hiyo washughulikiwe kisheria, anaejihusisha na suala la kuingiza mifugo hiyo kama itathibitika hawawezi kuwa na viongozi wanowahifadhi wahalifu wanaoingia Nchini bila kujali masilahi ya nchi na Ng'ombe zimekuwa kero kwa kuharibu Mashamba ya wananchi na Katika maeneo mengi ya hifadhi yameharibiwa sana na Wavamizi hao.

Alisema mpaka sasa mifugo yote iliyokamatwa kwa Nchi nzima ni mifugo 9500, na mifugo hiyo itatakiwa kutaifishwa baada ya Wanasheria na maafisa uhamiaji kuthibitisha kuwa iliingia kinyume cha sheria ili kuifanyia mnada na kukomesha wavamizi wote wanaoingia kinyume na utaratibu na kuharibu misitu na kuwa kichocheo cha migogoro ya wakulima na Wafugaji katika Maeneo ya vijijini.

Kwa upande wake kaimu Mkuu wa Wilaya ya kasulu ambae pia ni Mkuu wa wilaya ya Buhigwe, kanali Marco Gaguti alisema katika msako walioufanya wilayani humo wamefanikiwa kukamata Ng'ombe 1580 na kwamba mpaka sasa wanaendelea na oparesheni ya kusaka mifugo hiyo ilikuhakikisha ifikapo novemba10 mifugo hiyo iweimekwisha ondoka na kuhakikisha klhakuna mifugo mingine inayoendelea kuingia kinyume na utaratibu.

Aidha Mkuu huyo alisema ,wapo baadhi ya viongozi walioshirikiana na wafugaji kwa kupokea fedha na kuruhusu mifugo hiyo iendelee kuishi Nchini bila utaratibu, uchunguzi unaendelea kuwabaini na hatua za kisheria zitachukuliwa kwa wale watakao bainika na upelelezi unaendelea kufanyika kwa haraka kuhakikisha kuwa wamesafisha maeneo yote ambayo yamevamiwa na Wafugaji kutoka Nje na kuwabaini wale wote walioshirikiana nao.

Hata hivyo aliwaomba Wananchi kuendelea kutoa taarifa endapo kunawafugaji waliingia katika maeneo yao bila utaratibu na kuacha kuwahifadhi ilikuepusha migogoro ya Wafugaji na wakulima kutokana na wafugaji hao kuingilia maeneo ya wakulima.
 WAZIRI wa Mifugo na Uvuvi Luhaga Mpina akizungumza jambo na kaimu Mkuu wa Wilaya ya kasulu ambae pia ni Mkuu wa wilaya ya Buhigwe, kanali Marco Gaguti mara baada ya ukamataji wa Ng'ombe Wilayani kasulu Mkoani Kigoma
WAZIRI wa Mifugo na Uvuvi Luhaga Mpina akizungumza jambo na 
kaimu Mkuu wa Wilaya ya kasulu ambae pia ni Mkuu wa wilaya ya Buhigwe wakitafakari jambo kwa pamoja.

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages