Wanafunzi
waaliomaliza darasa la saba mwaka 2017 wa shule ya msingi ya New
Version wakiwa wamembeba mwanafunzi Lawrence Lucian aliyeongoza kwenye
matokeo ya Darasa la Saba shuleni hapo.
Shule
ya Msingi ya New Version ya Kibaha kwa Mathiasi imefanikiwa kung'aa
katika mtihani wa taifa darasa la saba mwaka huu kwa kushika nafasi ya
pili kiwilaya, nafasi ya tano kimkoa huku kitaifa ikishika nafasi ya 96
na kuwa na wastani wa 205. 1765.
Shule
hiyo ya New Vision kwa mwaka huu imepanda kutoka nafasi ya sita
iliyoshika mwaka jana katika mtihani wa taifa wa darasa la saba na kuwa
ya pili kiwilaya huku kimkoa ikishika nafasi ya 22 na kuwa ya 702
kitaifa huku ikiwa na wastani wa 163.0714.
Mkurugenzi
wa shule hiyo inayotoa elimu yake kwa lugha ya Kiingereza, Andrea
Mfuko alisema siri kubwa ya ufauli kwa watoto katika shule hiyo ni mfumo
mzuri wa ufundishaji na mazingira ya watoto kujisomea kwa utulivulisema
kwani kila Mwalimu anahakikisha kabla ya kuhama topic moja kwenda
nyingine ni lazima mtoto awe ameelewa vema, kile alichofundishwa.Amesema
mbali na masomo, Wanafunzi wa New vision wanafundishwa kujielewa,
kujitambua na kujua wajibu walionao kwa jamii inayowazunguka na taifa
kwa ujumla.
Kauli
mbiu ya shule hiyo yenye usajili namba PW.01/7/010 ni 'Education
brings self actualization' ambayo ina maono ya kutoa elimu bora na
kujenga jamii yenye kujitambua ambayo itakuwa ni sehemu muhimu ya
kutegemewa na taifa.
Aidha
amewaasa wazazi na walezi ili kufanya mtoto aweze kupata ufaulu mzuri
wametakiwa kutowabagua watoto katika mgawanyo wa kazi za nyumbani na
pia watambue wajibu wao wa kuwafuatilia watoto shuleni hasa pale
wanapoona hawaendi vizuri kwani elimu ya mtoto na ufaulu wake unategemea
sana jitihada za mzazi na mwalimu, iwapo kila mtu anatambua wajibu wake
na kumthamini mwenzake kwa nafasi yake.
Amewasihi wazazi kiwatia moyo watoto kutulia na kusoma kwa badii na kupenda zaidi masomo ya Sayansi.
Mfuko
alisema malengo yao makubwa ni kuendelea kufundisha kwa bidii sana ili
kuendelea kushika nafasi za juu katika mitihani ya kitaifa na kusaidia
watoto wengi wa Tanzania kupata elimu bora.
No comments:
Post a Comment