Shirika
la kimataifa la Save The Children limetoa msaada wa pikipiki kwa ajili
ya dawati la jinsia na watoto la jeshi la polisi wilaya ya Shinyanga kwa
ajili ya kukabiliana na vitendo vya ukatili wa kijinsia.
Akizungumza
leo Ijumaa Novemba 10,2017 wakati wa kukabidhi pikipiki moja kwa jeshi
la polisi,Meneja wa shirika la Save The Children mkoa wa Shinyanga
Benety Malima alisema pikipiki hiyo itasaidia katika ufuatiliaji wa
makosa mbalimbali yakiwemo ya jinai.
“Shirika
letu limekuwa likiendesha mafunzo kuhusu ukusanyaji wa vielelezo kwa
ajili ya uchunguzi wa kisayansi kwa ushahidi mahakamani,tumebaini kuwa
miongoni mwa changamoto zilizopo ni usafiri,kutokana na hali hiyo
tumeona tuangalie namna ya kuwezesha usafiri ili kukabiliana na vitendo
vya ukatili katika jamii”,alieleza Malima.
Akipokea
pikipiki hiyo SSP Lutusyo Mwakyusa aliyemwakilisha kamanda wa jeshi la
polisi mkoa wa Shinyanga ACP Simon Haule,alilishukuru shirika hilo kwa
kuona umuhimu wa kusaidia jeshi la polisi.
“Tunalishukuru
shirika la Save the Children, huu ni msaada mkubwa sana kwetu kwani
utasaidia kuokoa maisha ya watu,na hiki ni kielelezo tosha cha
ushirikiano kwa vitendo katika mapambano dhidi ya vitendo vya ukatili wa
kijinsia,naomba wadau wengine waige mfano wa shirika hili ili kujenga
jeshi letu la polisi”,alieleza Mwakyusa.
Aliwataka wadau kuendelea kushirikiana na jeshi la polisi ili kuhakikisha kuwa matukio ya ukatili yanatokomezwa.
Pikipiki
iliyotolewa na shirika la Save The Children kwa jeshi la polisi mkoa wa
Shinyanga ili itumiwea na dawati la jinsia na watoto kufuatilia matukio
ya ukatili wa kijinsia mkoani Shinyanga - Picha zote na Kadama Malunde
- Malunde1 blog
Meneja
wa Shirika la Save The Children Mkoa wa Shinyanga Benety Malima
akizungumza wakati wa zoezi la kukabidhi pikipiki kwa jeshi la polisi
mkoa wa Shinyanga kwa ajili ya dawati la jinsia na watoto.
Meneja
wa Shirika la Save The Children Mkoa wa Shinyanga Benety Malima
akikabidhi funguo ya pikipiki kwa mwakilishi wa kamanda wa polisi mkoa
wa Shinyanga SSP Lutusyo Mwakyusa
Meneja wa Shirika la Save The Children Mkoa wa Shinyanga Benety Malima akikabidhi funguo ya pikipiki kwa SSP Lutusyo Mwakyusa
Mwakilishi
wa kamanda wa polisi mkoa wa Shinyanga SSP Lutusyo Mwakyusa akijaribu
kuendesha pikipiki iliyotolewa na shirika la Save The Children.
No comments:
Post a Comment