Mhandisi
Robert Gabriel Mkuu wa Mkoa wa Geita akizungumza na wananfunzi wa Shule
ya Msingi Shinamwendwa (Halmashauri ya Mji Geita) alipokwenda kushiriki
kuchmba msingi wa ujenzi wa nyumba pacha ya Walimu shuleni hapo.
Akina
mama wa mtaa wa Machinjioni Kata ya Mgusu Halmashauri ya Mji Geita
wakishiriki katika ujenzi wa jengo la utawala kwa kubeba maji kupeleka
eneo la mradi.Wananchi wwameamua kujenga Shule ya Sekondari kwa kuwa
Kata hiyo haina hata shule moja hivyo watoto wanaofaulu ulazimika
kutembea umbali mrefu kufuata huduma ya elimu ya Sekondari katika Kata
za jirani.
Mhandisi
Robert Gabriel Mkuu wa Mkoa wa Geita akishiriki kujenga msingi wa
vyumba vya madarasa shule ya Sekondari Mgusu baada ya kuzindua kampeni
ya ujenzi wa vyumba vya madarasa na Zahanati Halmashauri ya Mji
Geita.Kata ya Mgusu inakabiliwa na changamoto ya kutokuwa na Shule ya
Sekondari.
Mhandisi
Modest Apolinary Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji Geita kitoa ufafanuzi
kuhusu ramani ya ujenzi wa Kituo cha Afya Kata ya Mgusu kwa Mkuu wa
Mkoa wa Geita Robert Gabriel kulia ni Herman Kapufi Mkuu wa Wilaya ya
Geita.
Mkuu
wa Mkoa wa Geita Mhandisi Robert Gabriel Luhumbi amemuagiza Mkurugenzi
wa Halmashauri ya Mji Geita Modest Apolinary kupeleka Wakaguzi wa ndani
wa Hesabu za Serikali Kata ya Mgusu ili wakakague na kujiridhisha na
mapato na matumizi ya fedha mbalimbali katika Ofisi ya Mtendaji wa Kata
ya Mgusu na Mtaa wa Machinjioni Wilayani Geita.
Mheshimiwa
Robert amesema hayo wakati wa ziara yake Halmashauri ya Mji Geita yenye
lengo la kuzindua kampeni ya ujenzi wa vyumba vya madarasa na Zahanati
ambapo baada ya uzinduzi kufanyika wananchi wa mtaa wa machinjioni
walimueleza kero ya kutopata taarifa ya mapato na matumizi ya michango
wanayochangia kwa ajili ya miradi ya maendeleo kwa muda mrefu katika
mtaa na kata ya Mgusu.
Akijibu
kero hiyo Mkuu wa Mkoa amesema "Kama kuna kiongozi wa mtaa au Kata
amekula fedha za wananchi hafai kuwa kiongozi serikali itamchukulia
hatua kali za kisheria na atarejesha fedha hizo!, Mkurugenzi leta timu
ya ukaguzi wa hesabu za Serikali ili ikague na kujiridhisha kama kuna
fedha yoyote iliyochukuliwa pasipo maelezo yanayojitosheleza hatua
zichukuliwe haraka kwa wote watakaobainika kuhusika".
Mheshimiwa
Robert ameongeza kuwa ukaguzi huo ufanyike kuanzia mwaka 2014 hadi 2017
kisha apate taarifa hiyo ofisini. Akiwa katika Halmashauri hiyo Mkuu wa
Mkoa amepongeza jitihada zinazofanywa na wananchi za kushiriki katika
utekelezaji wa miradi mbalimbali ya maendeleo licha ya kuwepo changamoto
nyingi katika maeneo yao.
Mkuu
wa Mkoa amehitimisha ziara yake ya Mkoa mzima katika Halmashauri ya Mji
Geita kwa kutembelea na kushirikiana na wananchi kujenga nyumba pacha
ya walimu (Two in one) Shule ya Msingi Shinamwendwa, ujenzi wa kituo cha
Zahanati Mtaa wa Nyakato , ujenzi wa vyumba vya madarasa viwili, ujenzi
wa jengo la utawala shule ya Sekondari Mgusu pamoja na kukagua eneo la
kujenga Zahanati katika Kata hiyo.
Katika
ziara hiyo ya Mkoa mzima Mheshimiwa Gabriel amefanikiwa kutembelea
Wilaya zote tano (5) na Halmashauri sita(6) na kufanikiwa kujenga,
kutembelea na kuanzisha jumla ya miradi 19 katika Sekta za Afya, Maji na
Ujenzi huku akikusanya zaidi ya mifuko 800 ya Saruji, tofali za Block
500, Mbao 50. Haya yote ni matokeo ya kazi aliyoianza ya kushirikiana na
wananchi kutekeleza miradi ya maendeleo katika kila kijiji ndani ya
Mkoa huu lengo kuu likiwa kuhakikisha wananchi wanapata huduma bora
karibu na maeneo yao pia kupunguza uhaba wa vyumba vya madarasa na
Zahanati Mkoa humu.
Wananchi
wote katika maeneo aliyopita kufanya kazi wameonyesha kuridhishwa na
utendaji kazi wa Serikali na kuamua kuunga mkono juhudi hizi kwa
kushiriki katika utekelezaji wa miradi kama vile kusoma maji, kubeba
mawe, mchanga, kokoto, kuchimba misingi na vijana kujitolea kujenga
miradi hii.
Na: Magesa Jumapili
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa
GEITA
No comments:
Post a Comment