Waziri
wa nchi ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora,
Mheshimiwa George Huruma Mkuchika amesema serikali itaendelea kuunga
mkono mchango wa Mfuko wa Maendeleo ya Jamii-TASAF katika kutatua kero
zinazowakabili wananchi katika kupambana na umasikini ili vita hiyo iwe
endelevu .
Mheshimiwa
Mkuchika amesema jambo muhimu kwa TASAF ni kuhakikisha kuwa walengwa
wote wa Mpango wa Kunusuru Kaya Masikini wanafikiwa na kunufaika na
huduma za mfuko huo huku akisisitiza juu ya umuhimu wa kuzingatia
maadili mema katika utendaji kazi wa wadau wote wanaohusika na
utekelezaji wa Mpango huo .
Akizungumza
baada ya kupokea taarifa ya utekelezaji wa shughuli za TASAF
zilizowasilishwa kwake na Mkurugenzi Mtendaji wa TASAF,Bwana Ladislaus
Mwamanga mjini Dodoma, Waziri Mkuchika ameuagiza uongozi wa TASAF
kuhakikisha kuwa unawatumia kikamilifu Maafisa maendeleo ya Jamii
walioko katika maeneo mbalimbali nchini kuhamasisha shughuli za
maendeleo na kupambana na umasikini.
“tunao
maafisa maaendeleo ya Jamii nchini kote,lakini nina wasiwasi na namna
wanavyotumiwa katika kutatua changamoto zinazowakabili wananchi,naagiza
TASAF mtumie vizuri hazina hiyo ya wataalamu katika utendaji kazi wenu”
ameagiza Waziri Mkuchika.
Aidha
Waziri huyo ameitaka menejimenti ya TASAF kuhakikisha kuwa inaandaa
mipango thabiti katika utoaji wa huduma kwa wananchi kwa kipindi kirefu
huku akisisitiza kuwa walengwa wa Mpango huo wanapaswa kuwekewa
mazingira yatakayowawezesha kujitegemea hata baada ya kuondolewa kwenye
shughuli za Mpango.
Akitoa
taarifa ya utekelezaji,Mkurugenzi Mtendaji wa TASAF ,Bwana Ladislaus
Mwamanga amesema mfuko huo umeendelea kuwajengea msingi wa kujitegemea
walengwa wa Mpango wa kunusuru kaya Masikini nchini kote,kazi ambayo
amesema imefanyika kwa mafanikio makubwa.
Walengwa
wengi hivi sasa wameweza kuanzisha miradi midogo midogo ya kiuchumi
kwenye maeneo yao huku akitaja mafanikio makubwa katika utekelezaji wa
masharti ya elimu na afya kwa walengwa jambo ambalo amesema linaendelea
kusaidia juhudi za serikali za kupambana na adua ujinga na maradhi.
“Kumekuwa
na mwitikio mkubwa katika kuwapeleka watoto kutoka kaya masikini kupata
elimu na huduma za afya, kwani hayo ni miongoni mwa masharti ya Mpango,
na hyo kwetu ni mafanikio makubwa” amesisitiza Bwana Mwamanga.
Hata
hivyo Mkurugenzi Mtendaji huyo wa TASAF amesema mfuko huo kwa sasa
unakabiliwa na changamoto ya kufikia takribani asilimia 30 ya vijiji
ambavyo havikufikiwa katika awamu inayokaribia kukamilika, hivyo
jitihada zaidi zinafanywa ili kupata fedha za kukamilisha vijiji hivyo
katika awamu itakayofuata.
Mheshimiwa
Mckuchika akitazama nakala za vipeperushi,taarifa na majarida yenye
taarifa za utekelezaji wa shughuli za TASAF,Ofisi kwake mjini Dodoma.
Waziri
Mkuchika (aliyevaa suti nyeusi) akiwa katika picha ya pamoja na baadhi
ya watendaji wa TASAF na Utumishi wa Umma ,baada ya kupata taarifa za
utekelezaji wa shughuli za TASAF ofisini kwake mjini Dodoma, aliyevaa
Kaunda suti ni Mkurugenzi Mtendaji wa TASAF,Bwana Ladislaus Mwamanga.
Waziri
wa nchi Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma,Mhe. George
Mkuchika (aliyevaa tai nyeusi) akipata maelezo kutoka kwa mkurugenzi
Mtendaji wa TASAF Bw. Ladislau Mwamanga,ofisi kwa Waziri mjini Dodoma.
No comments:
Post a Comment