Kampuni
za utengenezaji filamu za Mashauri Studios na Novitech kwa kushirikiana
na Clouds Plus pamoja na Shirikisho la Filamu Tanzania imezindua rasmi
mfumo wa kutengeneza, kutangaza, kuonyesha na kusambaza filamu za
kitanzania ujulikanao kama Bongohoodz.
Akizungumza
na waandishi wa habari, mwanzilishi mwenza wa Bongohoodz ambaye pia ni
mtayarishaji wa filamu na Mkurugenzi wa Mashauri Studios, Paul Mashauri,
mfanyabiashara ambaye katika miaka ya hivi karibuni alimua kuwekeza
katika filamu alisema Bongohoodz inakuja kuwasaidia waandaaji wa filamu
nchini kutatua tatizo la wizi wa kazi za sanaa hasa DVDs kutokana na
usambazaji wa sinema feki unaofanywa na baadhi ya wafanyabiashara wasio
waaminifu. “Baada ya kutoa sinema kazaa sokoni ikiwa ni pamoja na One
Month Date mwaka 2014, Maisha ni Siasa na Bongo na Fleva mwaka 2015
tumegundua kuwa wizi wa kazi za sanaa ‘piracy’ ni mkubwa sana.
Lakini
kupitia Bongohoodz, watayarishaji wa sinema nchini hawatahitaji tena
kusubiri mapato yao au uwekezaji wao urudi kwa kuuza DVDs, "Kimsingi
hata katika nchi zilizopiga hatua katika sinema unazungumzia Hollywood
(Marekani), Bollywood (India), China Film Industry (China) na Nollywood
(Nigeria), mapato makubwa yanatokana na uonyeshaji wa sinema katika
majumba ya sinema au ‘theaters’ wao wanaita ‘Box Office’.
Kwa
sababu wizi wa kazi za sanaa upo dunia nzima," alisema Mashauri na
kuongeza. "Lakini mapato ya kwanza wanayopata waandaaji wa sinema au
‘production houses’ yanatoka ‘Box office’ au katika nyumba za kuonyesha
sinema. Ndio maana sisi tutasema, kwanini tusionyeshe sinema hizi nchi
nzima katika matamasha makubwa ambapo watanzania watapata kuona sinema
zinazoburudisha na kufundisha kwa bei nafuu kabisa huku wakifurahia
vyakula mbalimbali, muziki, kisha filamu?”
Mashauri
alisema kuwa wameanza jitihada za makusudi za kutangaza sinema hizi
ikiwa ni pamoja na kuwatangaza wasanii na wazalishaji wa sinema,“Dunia
nzima waigizaji wenye majina makubwa ndio wanaovutia walaji au wanunuzi
wa filamu, hata kwetu imezoeleka hivyo.
Lakini
ili muigizaji awe mkubwa lazima kazi yake ionekana, "Kwa msingi huo na
kwa ushirikiano wa vyombo vya habari ikiwa ni pamoja na wadau wetu
Clouds Plus, tumeanzisha ‘reality show’ ijulikanayo kama ‘The Producers’
inayoruka Clouds Plus kupitia king’amuzi cha Azam Tv kila siku jumatatu
hadi ijumaa saa moja mpaka saa moja na nusu usiku na marudio siku ya
jumapili kuanzia saa nne asubuhi ambapo watanzania wataweza kuona namna
sinema zinavyotengenezwa na wasanii wanavyofanya kazi zao," alisema
Mashauri.
Mashauri
alisema kupitia kipiendi hicho watu mbalimbali ambao wanandoto za kuwa
waigizaji watajua nini wa natakiwa kufanya kwani wataona fursa ziliziopo
katika tasnia ya uigizaji na changamoto zinazowapata waandaji na
waigizaji. "Tunategemea kufanya kazi na waandaaji kumi kwa mzunguko wa
miezi sita sita na kila Producer atatakiwa kuzalisha sinema ndani ya
miezi sita na mchakato wa sinema yake utaonyeshwa katika reality show,
sinema yake itatangazwa na kupelekwa sokoni," alisema Mashauri.
Naye
Meneja wa Clouds Plus, Ramadhani Bukini, alisema Clouds Plus imeungana
na Bongohoodz katika kufanikisha ukuaji wa soko la filamu nchini kwa
kutoa fursa kwa wazalishaji wa sinema kuonyesha kazi zao na kuzipeleka
sokoni kupitia matamasha. “Tumeungana na Bongohoodz tukiamini kuwa
lazima kuwe na mbinu mbadala za kuuza sinema. Dunia imebadilika sana na
huwezi kutegemea chanzo kimoja cha mapato. Mfano, katika dunia ya leo,
aina ya kompyuta zinazoongoza kwa kuuza duniani ni za Apple.
Watumiaji
wa ‘computer’ hizi hawahamasiki kutumia DVDs. Inamaana tunakoelekea
hata wenye deki za kuangalia DVDs ni wachache, "Watu wako kwenye simu za
mikononi, ndio maana Clouds Plus ikaamua kuungana na Bongohoodz kuja na
vyanzo vipya vya mapato kwa tasnia ya filamu Tanzania ikiwa ni pamoja
na matamasha makubwa ya kuonyesha filamu. Kama imewezekana katika muziki
tunaamini kabisa inawezekana katika filamu," alisema Bukini.
Naye
mwanzilishi mwenza wa Bongohoodz ambaye pia ni mkurugenzi wa kampuni ya
Novitech ambayo inashirikiana na Mashauri Studios katika kutayarisha
sinema, Mary Mgurusi alisema watanzania wasubirie kwa hamu kazi nzuri za
filamu.
“Tumeandaa
sinema nzuri za kitanzania zenye maudhui tofauti tofauti ambazo
tunaamini zinaburudisha na kufundisha. Tayari sinema ya Tatu Chafu
imekamilika na tunatarajia kuizindua tarehe 16/12/2017 Mlimani City
pamoja na Dar Live Mbagala. Baada ya uzinduzi huo, tunatarajia kuonyesha
sinema hii nchi nzima katika mikoa mbalimbali. Zaidi ya Tatu Chafu zipo
sinema nyingi katika maandalizi, mfano Tajiri kutoka India, What is
Marriage, Rashid Snake Boy Matumla na School Bus," alisema Mgurusi.
No comments:
Post a Comment