Kampuni ya Uber ina furaha kuwatangazia
madereva wake wote kwamba imezindua vipengele vipya vyenye uwezo mkubwa
vitakavyowasaidia madereva kutoka kanda ya Afrika Mashariki kuwa na uhuru wa kuchagua maeneo, muda na namna
wangependa kuendesha gari kwenye mfumo wa Uber. Halikadhalika Uber imeongeza
mara dufu uwezo wa programu yake na kuifanyia maboresho makubwa.
Vipengele
hivi vipya vinakuja baada ya zana ya Kuchati Ndani ya Programu Iliyozinduliwa
hivi karibuni, kipengele kinachowasaidia madereva na wasafiri kuwasiliana kwa
kutumia programu ya Uber bila kuonesha namba zao za simu wanapotaka
kuwasiliana.
Meneja
Msimamizi wa Uber Nchini Tanzania, Alfred Msemo, anaelezea, "Siku zote sis
hufanyia kazi maoni ya madereva wetu ambayo hutusaidia katika kuboresha na
kuimarisha wigo wa madereva wanaotumia mfumo wetu. Madereva wanaotumia mifumo
yetu wameeleza wazi kuhusu kile wanachotaka na tumefanyia kazi maoni yao, kwa
hiyo tutazindua bidhaa ambazo zitasaidia kutafuta mwafaka katika sehemu tatu
kuu: kuwapa madereva uhuru zaidi hasa namna wangependa kutumia mfumo wa
Uber, kutumia teknnolojia kuwaondoleaa kero zozote wanazopata kazini,
pamoja na kuimarisha usalama.”
Kampuni
ya Uber itaanza kwa kuzindua bidhaa kadhaa ambazo madereva wameomba:
- Kuonesha Safari Yangu ya Dereva: Tayari Uber ina njia ambayo msafiri anaweza kuwaonesha watu wanaotaka alipofika kwenye safari yao yake, sasa kipengele cha Kuonesha Safari Yangu kinatoa nafasi kwa madereva kuonesha watu wa karibu maelezo ya safari yao, bila kuingilia faragha ya msafiri au kutoa taarifa ya kibinafsi au vituo vya kuchukua na kushusha abiria.
- Kituo na Muda wa Kuwasili: Sasa madereva wanaweza kuweka muda wanaotaka kuwasili mahali wanakoenda wakati wowote kwa kutumia kipengele cha Muda wa Kuwasili. Madereva wakiweka kituo na muda wa kuwasili, wanapoendelea na shughuli zao za kawaida programu itawakumbusha muda wa kuanza safari ukifika. Muda ukifika wataunganishwa na msafiri aliyeita gari kwenye barabara hiyo. Kipengele hiki kinawapa uhuru zaidi wa kujisimamia sambamba na kupata pesa zaidi wanapokuwa njiani kuelekea kituo wanachotaka.
- Arifa ya safari ndefu: Madereva watapata taarifa mapema itakayowajulisha kuhusu safari ya mwendo mrefu, hii ina maana kwamba madereva watajua mapema ikitokea kwamba safari itachukua dakika 45 au zaidi, ili wafanye maandalizi ya kutosha.
- Kulinda Ukadiriaji: Wakati mwingine wasafiri wanaweza kukadiria safari vibaya kutokana na sababu ambazo sio kosa la dereva kama vile hitlafu kwenye programu ya Uber. Sera mpya ya kumkadiria dereva, ukadiriaji wa aina hii hautajumuishwa kwenye jumla ya ukadiriaji wa dereva. Bado kampuni ya Uber itandelea kupokea maoni yatakayosaidia kuboresha huduma zake lakini hayataathiri wastani wa ukadiriaji wa dereva.
- Kitufe cha 'Hapana': Kipengele hiki kinawapa madereva uhuru wa kukataa safari bila hofu ya kwamba itaathiri mapato yao. Kwa sasa, madereva wanaweza kuthibitisha na kukubali safari au wasubirie muda wa ombi la usafiri uishe. Kipengele hiki kipya, cha kitufe cha 'hapana', kinawapa madereva uwezo wa kukataa safari mara moja - ni habari njema kwa wasafiri pia kwa sababu ombi litatumwa kwa dereva mwingine haraka hivyo hatapoteza muda mwingi akisubiria gari.
Ni
nini tafsiri yake kwa madereva? Msemo anafafanua, “Fatuma Mdee anapofungua
pprogramu na kuanza kukubali maombi ya wasafiri, anaweza kutumia kipengele cha
“Onesha Safari Yangu” kumtumia mume wake maelezo ya safari yake. Maelezo
haya ni kama vile mahali alikofika kwenye ramani. Ana uwezo wa kuanza
kumwonesha mume wake na watu wengine lakini anaweza pia kuacha kuwaonesha
maelezo ya safari yake muda wowote, na wanaweza kufuatilia mahali amefika bila
ugumu wowote kwenye ramani kwa kutumia maelezo yake ya namba ya simu na namba
pleti ya gari. ”
"Au
kwa mfano, dereva Omar Mohammed, ambaye ni baba wa watoto watatu na anatumia
programu ya Uber kumpa uhuru wa kusimamia maisha yake. Kitufe hiki kipya cha "Hapana", sasa
kinawapa madereva kama Omar uhuru zaidi wa kusimamia safari kwa sababu
kipengele hiki kinampa uwezo wa kukataa safari mara moja bila wasiwasi wowote
wa mapato yake kupungua. Hii ni habari njema kwa wasafiri pia kwa sbabu ombi la
usaifiri litatumwa moja kwa moja kwenda kwa dereva mwingine bila kupoteza muda
wowote.
"Tunajituma
kila siku kutumia uwezo wetu wa teknolojia na ofa zetu za madereva ili
kuwajengea madereva mazingira rafiki na wafurahie kazi yao wanapotumia mfumo wa
Uber. Tunaamini kwamba vipengele hivi vitaimarisha sio tu wigo wa madereva bali
maisha yo pia. "Amehitimisha Bw. Msemo.
Lakini
huu ni mwanzo tu - tumekusudia kuyapa kipaumbele maslahi ya dereva katika
mkakati wa Uber, Uber itaendelea kujituma ili kuimarisha wigo wa madereva
wanaotumia programu yetu. Maboresho haya si ya vipengele tu - ni sehemu ya
mkakati endelevu, na Uber ina furaha kubwa kutumia uwezo wake wa kiteknolojia
ili kuimairsha na kubadilisha wigo wa madereva 1,000 wanaotumia mfumo wa Uber
kila wiki.
No comments:
Post a Comment