MBUNGE
Wa viti maalum Mkoa Wa Iringa, Ritta Kabati ametoa wito kwa jamii
kuondoka na itikadi za kisiasa pindi linapokuja suala la maendeleo kwa
wananchi.
Akizungumza
na wazazi na walezi wa shule ya msingi Igeleke wakati wa ukarabati wa
madarasa ya shule hiyo mwishoni mwa wiki ikiwa ni ahadi yake ya
kukarabati shule za msingi zenye miundo mbinu mibovu na zamani, Kabati
alisema kuwa suala la ujenzi wa madarasa hauna siasa.
Alisema
kuwa maamuzi ya kukarabati shule za msingi lengo ni kuyaweka mazingira
bora ya kusomea wanafunzi na kuwaepusha na ajali zinazoweza kujitokeza
kutokana na uchakavu wa majengo.Kabati
alisema kuwa imekuwa kawaida pindi mtu akitaka kufanya maendeleo mambo
ya siasa yanaingizwa ila kwa serikali hii ya hapa kazi lazima tufanye
kazi za kuleta maendeleo kwa wananchi.
Aliongeza
kuwa maamuzi kufanya shughuli za kijamii hasa katika elimu ni kuifanya
jamii ya watu wa Iringa kuwa na Elimu iliyo bora na kuweza kuwa na
kizazi ambacho kitakuwa cha kimaendeleo kama ilivyo kanda za Kaskazini
ambapo elimu ni kipaumbele cha kwanza.
“Mimi
sipendi kuona watoto wa Iringa wanakuwa wafanyakazi wa kazi za ndani
kwa watu kwenye Pesa au wafanyakazi wengi najiuliza tu kwanini ile
Iringa ndio chimbuko la wafanyakazi wa kazi za ndani,nitapambana
kuhakikisha Iringa inakuwa na wasomi wengi ili kupunguza utegemezi na
kuondoa kasumba ya watu wengi wafanyakazi wa ndani ni kutoka mkoani
hapa”alisema
Kwa
upande wake mwenyekiti wa serikali ya mtaa wa Kihesa Kilolo B kupitia
chama cha demokrasia na maendeleo (CHADEMA) Eden Madembo alisema shule
hiyo inamiundombinu mibovu hivyo ni hatarishi kwa wanafunzi wa shule.Madembo
alisema kuwa haangalii itikadika ya vyama bali anatafuta viongozi walio
tayari kuleta maendeleo kwa kuwa hiyo ndio tija ya kuwa kiongozi
kuwatumika wananchi waliotuchagua wakati tukiomba kura za kuwa viongozi.
“Leo
hii mimi ni mwenyekiti wa CHADEMA lakini nipo na mbunge wa CCM
aliyekubali kuja kusaidia kuleta maendeleo katika shule yetu yaIgeleke
hivyo nipende kuweka wazi kuwa mimi kwenye maendeleo siangalii chama
gani kinaleta maendeleo”
Kabati (mwenye njano) akishirikiana na wananchi kubeba zege kwa ajili ya ukarabati wa shule ya msingi Igeleke
Kabati (mwenye njano) akishirikiana na wananchi kubeba zege kwa ajili ya ukarabati wa shule ya msingi Igeleke
Mbunge
wa viti maalum Ritta Kabati akikabidhi saruji kwa uongozi wa shule
kabla ya kuanza ukarabati katika shule ya msingi Igeleke.
No comments:
Post a Comment