Mkuu
wa wilaya ya Shinyanga Josephine Matiro leo Ijumaa Novemba 3,2017
amewatembelea wakulima wa zao la pamba katika kijiji cha Sayu kata ya
Pandagichiza halmashauri ya wilaya ya Shinyanga kwa ajili ya
kuwahamasisha kulima zao hilo kwa njia za kitaalamu/kisasa ili kilimo
hicho kiwe na tija kwa ajili ya kujikomboa kiuchumi.
Akizungumza
katika kikao na wananchi wa kijiji hicho ambacho ni maarufu kwa kilimo
cha pamba,Matiro aliyekuwa ameambatana na wataalamu wa zao la
pamba,aliwataka wakulima wa zao hilo wilayani humo kulima kisasa kwa
kufuata kanuni 10 za kilimo ikiwemo kulima kwa kutumia kamba.
Alisema
wananchi katika wilaya hiyo wamekuwa mstari wa mbele katika kulima zao
la pamba lakini wamekuwa hawapati faida kutokana na kulima njia zisizo
za kitaalamu.
“Tunataka
kufanya kilimo biashara ili kiwe na tija,hatupati mazao ya kutosha
kutokana na kutolima kitaalamu,naomba mwaka huu tuwasikilize wataalamu
wetu wanatuambia nini,nataka tubadilishe maisha yetu kupitia
pamba”,alisema Matiro.
Aliwashauri
wananchi ambao hawana uwezo wa kunua mbegu za pamba wajiorodheshe
majina yao,ijulikane wapo wangapi na wanahitaji mbegu kiasi gani ili
serikali ya wilaya hiyo ione namna ya kuwasaidia ili waweze kulima
kisasa.
“Tutaongea
na wadau wa pamba ili tujue tunafanya nini,sasa hivi tunaingia katika
msimu wa pamba,hatutaki pamba yetu kufanyiwa mambo yaliyokuwa
yanafanyika huko nyuma,tunataka tuwe na chama cha ushirika ili hata
tukiamua kuwapa mbegu wale walioshindwa waweze kupata kupitia chama chao
cha ushirika”,alieleza Matiro.
“Kijiji
hiki kinasifika kwa kilimo cha pamba na mazao mengine kama choroko na
dengu,naomba mujitahidi kufuata ushauri wa wataalamu wa kilimo lakini
msisahau kulima mazao ya chakula na muepuke kuuza chakula
chote”,alieleza.
“Serikali
haina shamba,jitahidini mnapolima mazao ya biashara limeni pia mazao ya
chakula na mhakikishe mazao yale mnahifadhi kwa ajili ya chakula cha
baadae”,aliongeza.
Aidha
aliwahamasisha wananchi hao kupanda miti ili kukabiliana na tishio la
jangwa mkoani Shinyanga ambapo kupitia kampeni ya Shinyanga Mpya,Mti
Kwanza kila kaya inatakiwa kupanda miti kuanzia mitatu.
Katika hatua nyingine aliwataka wataalamu wa kilimo kukaa na wakulima na kuwashauri njia nzuri za kufuata katika kilimo.Mmoja
wa wakulima katika kijiji hicho,Samwel Nkilijiwa alieleza kuwa tatizo
kubwa wanalokabiliana nalo kuwa ni pembejeo ambao dawa za maji
zinazotumika kuua wadudu hazijafanyi kazi kama ilivyokuwa kwa dawa za
mafuta ambazo sasa hazitumiki.
“Hii
dawa ya maji wanayotupa haiui wadudu wanaoshambulia pamba yetu,kwanza
inawasha sana huwezi hata kumsogelea mke wako,tunaomba ile dawa ya
mafuta tuliyokuwa tunaitumia zamani,hii haifai”,aliongeza Nkilijiwa.
Hata
hivyo Mkaguzi wa pamba wilaya ya Shinyanga,Benjamini Madama alisema
tatizo la wakulima kulalamikia dawa ya maji inatokana na kipindi cha
nyuma wafanyabiashara wa dawa hiyo walikuwa wanachakachua dawa hiyo na
kuonekana feki na sasa serikali imechukua hatua hivyo hakuna dawa feki
kinachotakiwa wakulima wafutae ushauri wa wataalamu wa pamba.
Mkuu
wa wilaya ya Shinyanga Josephine Matiro akizungumza na wananchi wa
kijiji cha Sayu kata ya Pandagichiza leo akiwahamasisha kufuata njia za
kisasa kulima zao la pamba-Picha zote na Kadama Malunde - Malunde1 blog
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Josephine Matiro akizungumza na wananchi wa Sayu
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Josephine Matiro akisisitiza wananchi kulima mazao ya biashara pamoja na yale ya chakula
Wananchi wakimsikiliza mkuu wa wilaya ya Shinyanga
Mkulima wa Pamba Nicholaus Selena akieleza kero yake kwa mkuu wa wilaya ya Shinyanga Josephine Matiro
Mkulima
wa Pamba Samwel Nkilijiwa akieleza changamoto wanayopata pale
wanapotumia dawa ya maji ya kuua wadudu ambapo alisema dawa hiyo haiui
wadudu hivyo kuomba dawa ya mafuta waliyokuwa wanatumia zamani
Afisa Kilimo wa wilaya ya Shinyanga Edward Maduhu akitoa ufafanuzi kuhusu kilimo cha pamba
Diwani wa kata ya Pandagichiza Charles Masele Kabogo akizungumza katika kikao hicho
Afisa tawala wa wilaya ya Shinyanga Charles Maugira akizungumza katika kikao hicho
Mkulima
wa pamba katika kijiji cha Sayu Ezekiel Nchange akishikana mkono na
mkuu wa wilaya ya Shinyanga Josephine Matiro baada ya kumpatia shamba
mkuu huyo wa wilaya ili alime zao la pamba katika kijiji hicho
Mkaguzi
wa pamba wilaya ya Shinyanga,Benjamini Madama akitoa elimu kwa wakulima
wa pamba juu ya njia ya kisasa ya kulima zao hilo
Mkaguzi wa pamba wilaya ya Shinyanga,Benjamini Madama akionesha kamba zinazotakiwa kutumika katika kilimo cha pamba
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Josephine Matiro akipokelewa katika shule ya msingi Sayu kwa ajili ya kupanda mti
Mkuu
wa wilaya ya Shinyanga Josephine Matiro akipanda mti wa kumbukumbu
katika shule ya msingi Sayu ikiwa ni sehemu ya utekelezaji wa kampeni ya
Shinyanga Mpya Mti Kwanza ambapo wananchi wamekuwa wakihamasishwa
kupanda miti ili kukabiliana na hali ya jangwa mkoani Shinyanga
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Josephine Matiro akiendelea na zoezi la kupanda mti katika shule ya msingi Sayu
Mkuu
wa wilaya ya Shinyanga Josephine Matiro akizungumza na wanafunzi wa
shule ya msingi Sayu ambapo aliwasisitiza kuwa mabalozi wa upandaji miti
katika jamii
Mkuu
wa wilaya ya Shinyanga Josephine Matiro akizungumza na baadhi ya
viongozi na wananchi wa kijiji cha Bulambila kata ya Mwalukwa ambapo pia
ni maarufu kwa kilimo cha zao la pamba ambapo pia aliwahamasisha kulima
zao hilo kwa njia za kisasa ili lilete tija
Mkuu
wa wilaya ya Shinyanga Josephine Matiro akiteta jambo na Diwani wa kata
ya Mwalukwa,Ngassa Mboje ambaye pia ni mwenyekiti wa halmashauri ya
wilaya ya Shinyanga Vijijini.
No comments:
Post a Comment