Wanafunzi
wa Shule ya Msingi ya Shila Wilayani Nzega mkoani Tabora wakiwa
wamebeba mbegu ya Viazi lishe wakielekea kwenye shamba darasa wakati wa
uzinduzi wa shamba hilo wilayani humo leo. Shule hiyo ni shule pekee
wilayani humo kupata bahati ya kuanzisha shamba hilo.
Mwakilishi
wa Kaimu Mkurugenzi wa COSTECH ambaye ni Ofisa Mwandamizi wa COSTECH,
Audax Mutagwa (kulia), akimkabidhi mbegu ya mihogo Mkuu wa Wilaya ya
Nzega, Godfrey Ngapula kwa ajili ya kupandwa katika mashamba darasa
katika uzinduzi wa mashamba hayo ya mbegu wilayani humo leo.
Wanafunzi wa Shule ya Shila wakiwa shambani wakati wa uzinduzi wa shamaba darasa hilo.
Ofisa
Kilimo kutoka Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Tabora, Said Babu akizungumza
kabla ya kuanza uzinduzi huo uliofanyika katika Wilaya hiyo Shule ya
Msingi, Shila.
Mwakilishi wa Kaimu Mkurugenzi wa COSTECH ambaye ni Ofisa Mwandamizi wa COSTECH, Audax Mutagwa, akizungumza katika uzinduzi huo.
Mtafiti
wa mazao ya mizizi kutoka Kituo cha Utafiti wa Kilimo cha Maruku mkoani
Kagera, Jojianas Kibura, akielezea ubora wa mbegu ya mihogo
iliyofanyiwa utafiti kabla ya uzinduzi wa shamba darasa katika Shule ya
Msingi ya Shila.
Kaimu Ofisa Ugani wa Halmshauri ya Wilaya ya Nzega, Hassan Mtomekela akizungumza katika uzinduzi huo.
Mtafiti
wa mazao ya mizizi kutoka Kituo cha Utafiti wa Kilimo cha Maruku mkoani
Kagera, Jojianas Kibura, akielekeza jinsi ya kupanda mbegu ya mihogo
hiyo kiutaalamu.
Mtafiti
wa mazao ya mizizi kutoka Kituo cha Utafiti wa Kilimo cha Maruku mkoani
Kagera, Jojianas Kibura, akimuonesha mbegu hiyo mkuu wa wilaya hiyo.
Mkuu wa Wilaya hiyo akizindua shamba darasa hilo kwa kupanda mbegu ya mihogo katika Shule ya Msingi ya Shila.
Mwalimu Mkuu wa Shule hiyo, Gunguti Awadh Mzee akipanda mbegu hiyo.
Dada Mkuu wa Shule ya Shilwa, Maria Kulwa akipanda mbegu hiyo.
Upandaji ukiendelea katika shamba hilo.
Mwalimu
Mkuu wa Shule hiyo, Gunguti Awadh Mzee, akizungumza na waandishi wa
habari kuhusu bahati iliyopata shule yake kwa kupatiwa mradi huo wa
shamba la mbegu.
Mkulima wa Kijiji cha Shila, Zainabu Kanijo akizungumza na wanahabari.
Wanawake
wa Kikundi cha Wasafi Camp Imala Makoye kilichopo Kijiji cha Iyombo
Kata ya Utwigu wakiwa wamebeba mbegu ya Viazi lishe wakielekea kupanda
katika shamba darasa.
Mtafiti
wa mazao ya mizizi kutoka Kituo cha Utafiti wa Kilimo cha Maruku mkoani
Kagera, Jojianas Kibura, akiwaelekeza wanakikundi hicho jinsi ya
kupanda mbegu hiyo.
Wanawake
wa Kikundi cha Wasafi Camp Imala Makoye kilichopo Kijiji cha Iyombo
Kata ya Utwigu wakipanda mbegu hiyokatika shamba lao.
Wanawake
wa Kikundi cha Wasafi Camp Imala Makoye kilichopo Kijiji cha Iyombo
Kata ya Utwigu wakiimba nyimbo za kabila la kisukuma kufurahi mbegu
hiyo.
Mtafiti
wa mazao ya mizizi kutoka Kituo cha Utafiti wa Kilimo cha Maruku mkoani
Kagera, Jojianas Kibura, akiwaelekeza wakulima wa Kijiji cha Upungu
Kata ya Puge jinsi ya kupanda mbegu ya mihogo
Na Dotto Mwaibale, Nzega Tabora
MKUU wa Wilaya ya Nzega mkoani Tabora, Godfrey Ngapula amesema Sayansi na Teknolojia haiwezi kuepukika katika kilimo nchini.
Ngapula
ameyasema hayo leo kwenye uzinduzi na kukabidhi mbegu bora za Mahindi
ya Wema 2109, mihogo na Viazi lishe kwa ajili ya kuanzisha mashamba
darasa katika vijiji vya Shila, Iyombo, Upungu, Lububu na Kapanga
wilayani humo.
Mkuu
huyo wa wilaya alisema ili kufanya kilimo chenye tija sayansi na
teknolojia haiwezi kuepukika kutokana na changamoto mbalimbali zilizopo.
Alisema
kilimo cha kisayansi kina tija kwani mkulima anaweza kulima eneo dogo
na kupata mavuno mengi kuliko kilimo cha mazoea ambacho mkulima hulima
shamba kubwa mazo kidogo.
Ngapula
aliipongeza Tume ya Taifa ya Sayansi na Teknolojia (COSTECH) kwa
kuwapelekea mbegu hizo kwa kushirikiana na Jukwaa la Bioteknolojia kwa
Maendeleo ya Kilimo (OFAB)
Akizungumzia
matumizi ya mbegu zilizozalishwa kwa teknolojia ya uhandisi jeni (GMO)
alisema hayakwepeki kwa kuwa mbegu hizo zinasifa ya kukabiliana na
changamoto mbalimbali ikiwemo ukame na wadudu waharibifu wa mazao.
Alisema
wilaya hiyo kupelekewa mbegu hizo kwao ni fursa kubwa na kwa
kushirikiana na wakulima na maofisa ugani atahakikisha mashamba darasa
hayo yanatunzwa vizuri na kuwa ndio chanzo za kutoa mbegu nyingi na
kuzisambaza katika maeneo mengine.
Mtafiti
wa mazao ya mizizi kutoka Kituo cha Utafiti wa Kilimo cha Maruku mkoani
Kagera, Jojianas Kibura aliwaambia wakulima hao kuwa hekta moja ya
mihogo iwapo watalipa kwa kufuata ushauri wa wataalamu wataweza kupata
tani 25 hadi 32 kwa zao la mihogo na viazi lishe watapata tani 7 hadi 9
kwa hekta moja.
Alisema
matokeo hayo watayapata endapo watafuata kanuni bora za kilimo cha
mazao hayo kwa kuzingatia nafasi kati ya mche na mche na mstari kwa
mstari na matumizi ya mbolea hivyo wataweza kuongeza uzalishaji zaidi
tofauti na sasa ambapo kwenye hekta moja ya mihogo wanapata tani nane
hadi kumi wakati kwenye viazi lishe wanapata tani moja hadi 3.
Mtafiti
huyo alisisitiza kuwa mbegu hiyo ya Mihogo ya Mkombozi imefanyiwa
utafiti na kuonekana kustahimili magonjwa hatari ya mihogo ya batobato
kali na michirizi ya kahawia ambayo imekuwa ikiwapatia hasara kubwa
wakulima wengi na kupoteza hadi asilimia 90 za mazao.
Akizungumzia
kuhusu mbegu Mwakilishi wa Kaimu Mkurugenzi wa COSTECH ambaye ni Ofisa
Mwandamizi wa COSTECH, Audax Mutagwa, alisema mbegu hizo ya mihogo aina
ya Mkombozi imefanyiwa utafiti na kuonekana ina uwezo mkubwa wa
kustahimili magonjwa kama ya batobato kali na michirizi ya kahawia
ambayo imekuwa ikiwapatia hasara kubwa wakulima na ya mahindi
ikistahimili hali ya ukame na kutoa mazao mengi.
Mutagwa
aliwaomba wakulima hao kuyatunza mashamba hayo ambayo yamegharimu fedha
nyingi hadi kukamilika kwake hivyo wayaendeleze kwa ajili ya kuja kutoa
matunda kwa wakulima wa wilaya hiyo na kupata chakula cha kutosha na
ziada kuuza.
Aliongeza
kuwa kazi kubwa ya COSTECH ni kuishauri serikali katika masuala
mbalimbali ya sayansi na teknolojia na kuhakikisha matokeo ya tafiti
zinazofanyika nchini yanawafikia walengwa ambao ni wakulima.
Mwalimu
Mkuu wa Shule ya Msingi ya Shila ambayo ni shule pekee iliyopata baada
ya kuwa na shamba darasa la mihogo katika wilaya hiyo, Gunguti Awadh
Mzee alisema shamba hilo litakuwa la mfano na kuwa mradi huo utasaidia
kuwapatia wanafunzi wake chakula wakiwa shuleni hapo.
No comments:
Post a Comment