Mawakala wa Kampuni ya BCX
wakiwa katika picha ya pamoja wakijiandaa kutoa elimu ya jinsi ya kutumia mfumo
mpya wa kielektroniki wa malipo ya nauli katika usafiri wa Daladala kwa kutumia
Kadi au Stika kwa abiria wa eneo la Feri zoezi lililofanyika hivi karibuni jijini
Dar es Salaam.
Dereva wa Daladala, Abdallah
Kombo akigawa vipeperushi kwa Abiria vinavyoelezea namna ya kutumia mfumo mpya
wa malipo ya nauli kielektroniki katika usafiri wa Daladala, uliozindulwa hivi
karibuni na Kampuni ya BCX jijini Dar es salaam.
Mawakala wa Kampuni ya Business
Connexion (BCX), wakiwahudumia wateja wa huduma mpya ya malipo ya nauli za
daladala kielektroniki ijulikanayo kama ‘Uhuru Pay’ katika Kituo cha daladala
cha Tegeta Nyuki hivi karibuni jijini Dar es Salaam.
Wakala wa Kampuni ya Business
Connexion (BCX), akiwakabidhi vipeperushi wakazi wa Tegeta Nyuki, ambavyo
vinatoa maelezo kuhusu huduma mpya ya malipo ya nauli za daladala kielektroniki
ijulikanayo kama ‘Uhuru Pay’ iliyozinduliwa na BCX hivi karibuni jijini Dar es
salaam.
Mkazi wa Tegeta Nyuki, Bi. Leila
Msagar akipewa maelezo kabla ya kusajiliwa na kupewa kadi yake wakati wa
uzinduzi wa huduma mpya ya malipo ya nauli za daladala kielektroniki
ijulikanayo kama ‘Uhuru Pay’ ambayo ilizinduliwa na BCX hivi karibuni jijini
Dar es salaam.
No comments:
Post a Comment