Meneja
Uhusiano wa AIRTEL Tanzania Jackson Mmbando akizungumza na waandishi wa habari
leo katika uzinduzi wa programu mpya ya
Airtel U900 ambao lengo lake kuu ni kuimarisha ubora wa mtandao na kutoa
huduma bora kwa wateja wake mahali popote nchini. Mradi Tayari ushazinduliwa na
kuwasha mitambo kwenye mikoa ya Dar es Salaam, Mwanza na Arusha. Kulia ni
Meneja Ubora wa huduma za Mtandao Emmanuel Luanda
uzinduzi huo umefanyika katika makao makuu ya kampuni hiyo jijini Dar es Salaam.
uzinduzi huo umefanyika katika makao makuu ya kampuni hiyo jijini Dar es Salaam.
Meneja Ubora wa huduma za
Mtandao wa Airtel Tanzania Emmanuel Luanda (kulia) akiongea na waandishi wa habari
jijini Dar es Salaam baada ya kuzindua programu mpya ya Airtel U900 ambao lengo
lake kuu ni kuimarisha ubora wa mtandao na kutoa huduma bora kwa wateja wake
mahali popote nchini. Kushoto ni Meneja Uhusiano wa kampuni hiyo Jackson
Mmbando. Teknolojia hii itaongeza upatikanaji wa
mtandano wa 3G kwa Asilimia 50 zaidi pamoja na kuongeza ubora wa upatikaniji wa
intaneti bila kujali maeneo mteja alipo uzinduzi huo umefanyika katika makao makuu ya kampuni hiyo jijini Dar es Salaam.
Meneja Chapa na Masoko
Airtel Tanzania Anorld Mandale (katikati) akizungumza na waandishi wa habari baada ya kuzindua programu mpya ya Airtel U900 ambao lengo lake kuu ni
kuimarisha ubora wa mtandao na kutoa huduma bora kwa wateja wake mahali popote
nchini. Kampuni hiyo pia huduma ya Bando la OFA KABAMBE
ambapo wateja wataweza kufaidi huduma hii kwa kupiga *150*60# na
kujipatia 1GB, dakika150 kwa muda wa siku saba uzinduzi huo umefanyika katika makao makuu ya kampuni hiyo jijini Dar es Salaam.
Meneja Chapa na Masoko
Airtel Tanzania Anorld Mandale (katikati) akishika bango pamoja na maofisa wenzake wa kampuni hiyo baada ya kuzindua huduma ya Bando la OFA KABAMBE ambapo wateja wataweza kufaidi
huduma hii kwa kupiga *150*60# na kujipatia 1GB, dakika150 kwa muda wa
siku saba. Kushoto ni Meneja Ubora
wa huduma za Mtandao wa Airtel Tanzania Emmanuel Luanda na Meneja Uhusiano
Airtel Tanzania Jackson Mmbando
Teknolojia ya U900 kuwapatia watumiaji wa Airtel Intaneti yenye kasi popote
Teknolojia ya U900 kuwapatia watumiaji wa Airtel Intaneti yenye kasi popote
•Airtel yawekeza kwenye teknolojia mpya ya intaneti kutoa mtandao bora hata ukiwa ndani ya jengo.
Airtel
Tanzania Plc kampuni ya mawasiliano iliyojikita katika huduma zenye
ubunifu wa teknolojia zaidi nchini, leo katika muendelezo wake wa
kutimiza dhamira yake ya kuwa mtandao bora zaidi imetangaza na kuzindua
rasmi programu yake ya maboresho ya huduma za mtandao wake kupitia
teknolojia ya iliyopewa jina la ‘Mradi wa U900’ ukiwa na lengo la kuimarisha ubora wa mtandao na kutoa huduma bora kwa wateja wake mahali popote nchini.
Mradi
wa U900 ni uwekezaji mkubwa unaolenga kuhakikisha uhakika wa
upatikanaji wa huduma ya 3G, ujazo wa data kamili pamoja na kuongeza
kasi ya intaneti kwa kutumia teknolojia hii ya mawimbi ya mawasiliano ya
masafa ya 900 Mhz. Teknolojia hii itaongeza upatikanaji wa mtandano wa
3G kwa Asilimia 50 zaidi pamoja kuongeza ubora wa upatikani wa intaneti
bila kujali maeneo mteja alipo, Popote utapata Intaneti bora.
Akiongea
leo jijini Dar es Salaam wakati wa kutangaza huduma hiyo, Meneja huduma
wa mtandao Airtel Bw, Emanuel Luanda alisema kuwa Airtel imewekeza
kwenye kuimarisha huduma ya mtandao kutokana na ongezeko la matumizi ya
simu za smartphone na pia kutokana na uhitaji wa huduma mpya za ziada.
Kutokana na uboreshaji wa mtandao wetu, wateja wote nchini watakuwa
wakitapa huduma yenye kasi na hivyo kuwa na uhakika na huduma bora
kutoka Airtel wakiwa popote.
Bw,
Luanda alidokeza “ripoti ya hivi karibuni ya TCRA inayotoa mchanganuo
wa matumizi ya huduma za Intaneti (Data) inaweka wazi kuweko kwa
ongezeko la watumiaji wa huduma za intaneti kutokea 34% kwa mwaka 2015
na kupaa hadi 40% kwa mwaka 2016. Hali hiyo ndio inatoa msukumo hata
kwetu Airtel kuendelea kuwekeza zaidi katika teknolojia mpya ili
kuwapatia wateja wetu huduma bora zaidi”.
“Tayari
tushafanya maboresho kwenye miji ya Dar es Salaam, Arusha na Mwanza
huku maboresho mengine yakiendelea kufanyika Dodoma, Morogoro na miji
mingene yenye uhataji mkubwa wa huduma zetu hapa Tanzania.” Alieleza
Luanda
Kwa
upande wake, Meneja wa Masoko Airtel Tanzania Arnold Madale alisema,
“kwa kuwa Airtel tunatambua mahitaji ya wateja wetu, hali ya soko
tumekuwa tukifanikiwa kuleta bidhaa zenye ubunifu na mpangilio wa
huduma zinazozingatia mahitaji ya mteja, hii ni hatua kubwa sana hasa
kwenye ushindani wa biashara. Tunao wateja ambao wanatumia mtandao wetu
kwa ajili ya intaneti tu, lakini pia kuna wale wanaotumia kwa kupiga na
kupokea simu, tunazo bidhaa na huduma ambazo zinakidhi matakwa ya
wateja hao kwa muda wote wakiwa mahali popote. Kwa sasa hivi tunaendelea
pia kuboresha huduma yetu ya 2G ili kutoa huduma yenye uhakika wa hali
ya juu ikiwemo huduma ya Airtel Money ili kuendelea kuwafikia Watanzania
wengi waishio pembezoni huduma za kibenki na huku tukitimiza sera ya
serikali ya kushiriki katika uboreshaji wa huduma bora za kifedha
vijijini.”
“Tunapotangaza
huduma hii muhimu ya kuboresha mtandao wetu, tunayo furaha kutangazia
huduma ya Bando la OFA KABAMBE ambayo inapatika kwa urahisi na kumfanya
mteja kuwa na Uhuru zaidi wa kutumia Intaneti yenye kasi kwa muda mrefu
zaidi kwa kuwasiliana na ndugu, marafiki au wadau katika biashara
mahali popote. Wateja wetu wataweza kufaidi huduma hii ya bando kwa
kupiga *150*60# na kujipatia 1GB, dakika150 kupiga mitandao yote na
kudumu nazo kwa muda wa siku saba, aliongeza Madale.
‘Nia
yetu ni kuendelea kukua kupita Maelezo huku tukitengeneza ujuzi wa
kuaminiwa na wateja wetu kwa kuwa na gharama nafuu. Mradi wa U900
unadhihirisha kuwa Airtel imeamua kuinua taifa letu kufikia lengo la
kuishi kidigitali kwa kuwepo na huduma za kidigitali, aliongeza Madale.
No comments:
Post a Comment