A great place to access the latest news and information.

Breaking

Post Top Ad

Your Ad Spot

Tuesday, September 19, 2017

SHULE YA AL MUNTAZIR YAFANYA MAHAFALI YA KUWAAGA DARASA LA SABA

Kamishina Mkuu wa Skauti Tanzania Abulkarim Shah amesema kuwa watahakikisha wanapambana na suala la mimba za utotoni kwa wanafunzi wa shule za Almuntazir na taifa kwa ujumla ili wanafunzi waweze kupata elimu bora na kutimiza ndoto zao.
Kamishina Mkuu Shah ameyasema hayo leo katika mahafali ya shule ya Al-Muntaziir Boys Primary School jijini Dar es Salaam, ambapo ameeleza kuwa mimba hukatiza masomo ya wanafunzi wengi, hivyo hawana budi kupambana ili watoto wengi waweze kupata elimu bora na kutimiza malengo yao.
Katika hatua nyingine Shah amehimiza ushirikiano baina ya wazazi na uongozi wa shule ili kuchochea maendeleo ya wanafunzi na waweze kukuza taaluma zao, pia hii itasaidia kujua mienendo ya wanafunzi.
Kwa upande wake Mkurugenzi wa Al-Muntazir ambaye ni msimamizi wa shule zote za Al-Muntazir Mahmood Ladak ameiomba serikali kuendelea kushirikiana na sekta binafsi ili kuchochea maendeleo ya elimu, huku akimpongeza Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda kwa kuendelea kushirikiana nao kwa hali na mali katika kuhakikisha elimu inakuwa bora kwa watanzania wote.
Ladak ameleza kuwa wanafunzi 300 wanataraji kuhitimu siku ya leo, huku akifafanua kuwa anaimani kubwa ya ufaulu kwa wanafunzi hao kwani shule za Almuntazir zinatoa elimu bora na gharama zake ni  nafuu kulingana na haku ya kiuchumi ya watanzania wa hali ya chini.
"Jumla ya wanafunzi wa shule za Almuntazir ni 2000 lakini wanaomaliza leo ni 300 kwa wavulana na wasichana, imani yetu ufaulu utakuwa mkubwa kutokana na elimu bora na nafuu tunazo zitoa, ambapo kwa muhula unaokuja haitazid milioni 3 kwa mwaka" Alisema Ladak

Lawena Mfinanga ni mmoja wa wanafunzi wanaohitimu siku ya leo ambaye amewahimiza wanafunzi wenzake wanaobaki kusoma kwa bidii kwani, bila kufanya hivyo hawawezi kutimiza ndoto zao.

Salum Kabethi ni Afisa Elimu wa Kata ya Kivukoni amepongeza maendeleo ya shule za Al-Muntazir huku akizitaka shule zingine kuiga mfano huo kwa maendeleo ya elimu na kuhimiza ushirikishwaji wa wazazi katika shuguli za maendeleo ya shule.

Licha ya zawadi zitakazo tolewa siku ya leo kwaajili ya wanafunzi waliofanya vyema, Suleiman Salehe ambaye ni mmoja wa wazazi amesema atatoa zawadi ya vitabu kwa shule hiyo ilikuchochea maendeleo maendeleo ya elimu shuleni hapo.
"Nitatoa vitabu kuchochea maendeleo ya elimu lakini pia mtoto wangu Sabri anasoma hapa alikuja kwa uhamisho akitokea nchini Marekani na ameweza kufanya vyema hivyo natoa pongezi za dhati kwa shule hii" Alisema
 

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages