Kuelekea Ndanda Day kesho, Timu ya Soka ya Ndanda inatarajia kushuka dimbani kuumana na Kikosi cha Azam katika kuadhimisha siku hiyo kwenye Uwanja wa Chamazi, Jijini Dar es salaam.
Mchezo huo utakaoanza sa 10 alasiri utatanguliwa na burudani mbalimbali ikiwemo muziki kutoka kwa wasanii wa bongo flava wenye asili ya Mkoani Mtwara.
Akizungumza kuelekea maadhimisho ya siku hiyo, Afisa habari wa Ndanda Idrisa Bandari amesema kuwa katika siku ya kesho wataanza asubuhi kwa kwenda kutoa huduma za kijamii hospitali ya Temeke wodi ya wazazi na kisha kufuatiwa na burudani kutoka kwa wasanii wa muziki wa bongo Flava.
Bandari amesema, wasanii hao Wenye asili ya mkoani Mtwara Jay Mo, Amini, TID, Msaga Sumu na Juma Nature anayetokea Mkoa wa Pwani ambapo watatanguliza shughuli hiyo inayofanyika kwa mara ya nne ambapo mwaka huu itakuwa Mkoa wa Dar es salaam ikiwa ni mara ya kwanza.
Kwa upande wa Mshauri Masoko wa Ndanda, Peter Simon amesema kuwa kwa mwaka huu Ndanda Day itafanyika mara mbili kwani wameamua kuifanya na Dar es salaam kwani wanaamini kuna mashabiki wengi sana ndani ya Mkoa huu pia ili kuwapa fursa mashabiki wao kuiona Ndanda mpya iliyo chini ya Kocha Ramadhan Nsanzalwino mwenye asilia ya Burundi.
Meneja Mkuu wa Masoko wa Mitsun Group ambao ni wadhamini wa Ndanda, Erhad Mlyansi amewaahidi uongozi wa Ndanda kuwapatia bidhaa kutoka kampuni yao ya Sayona kwa ajili ya kuwapelea wagonjwa siku ya kesho.
Nao Wasanii wamewataka mashabiki wa Ndanda kujitokeza kwa wingi siku ya kesho kwa ajili ya kuishuhudia timu yaon na kwa mwaka huu wanaamini kutokana na udhamini walioupata basi timu yao ya Mkoani Mtwara itafanya vizuri huku wakiahidi kutoa burudani ya kutosha.
Afisa habari wa Ndanda, Idrisa Bandari akizungumza na wanahabari kuelekea Ndanda Day itakayoadhimishwa kesho katika Uwanja wa Chamazi wakicheza na timu ya Azam Fc ikiwa ni mara ya nne kufanyika kwa Tamasha hilo na likisindikizwa na burudani kutoka kwa wasanii wa Bongo Flava wenye Asili ya Mkoani Mtwara pamoja na kutoa huduma za kijamii katika Wodi ya wazazi Hospital ya Temeke. Kushoto ni mshauri wa Masoko wa Ndanda Peter Simon akifuatiwa na wasanii wa Bongo Flava Jay Mo, Richie One na Amini.
Meneja Mkuu wa Masoko wa Mitsuni Group,Erhard Mlyansi amewaahidi Ndanda kuwapatia bidhaa zinazopatikana kutoka kampuni ya Sayona kwa ajili ya kuwapelekea wakinamama kwenye Wodi ya wazazi Temeke Hospital siku ya Kesho
Msanii wa Muziki wa Kizazi kipya Khaleed maarufu kama Top In Dar 'TID' akihamasisha mashabiki wa wana Mtwara kujitokeza kwa wingi siku ya kesho Kuadhimisha Ndanda Day akiwa sambamba na wasanii wenzake Jay Mo, Richie One na Amini.
No comments:
Post a Comment