A great place to access the latest news and information.

Breaking

Post Top Ad

Your Ad Spot

Sunday, August 20, 2017

RC MAKONDA AWEKA MKAKATI WA KUBORESHA BARABARA ZA DSM

Mkuu wa Mkoa wa Dar es Samaam Paul Makonda, akiongea na  waandishi wa habari pamoja na washiriki waliojitokeza kwa wingi kwenye kongamano la tathmini ya hali ya miundombinu ya barabara katika Mkoa wa Dar es Salaam hafla hiyo ilifanyika katika ukumbi wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini hapa mapema leo.

*MKAKATI WA KUBORESHA BARABARA ZA DAR ES SALAAM*
Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam *Paul Makonda* leo amefanya Kongamano la tathimini ya hali ya miundombinu ya Barabara kwenye Mkoa wake ambapo ameendelea na msimamo wa kutoruhusu Kampuni za ujenzi za *Del Monte* na *Skol Building Contraction*kufanya kazi katika Mkoa wake.

*Makonda* amesema kuwa Kampuni yoyote itakayofanya Ujenzi wa Barabara chini ya kiwango atahakikisha inawajibishwa kwakuwa makampuni kama hayo ndio yanayochangia Barabara kuharibika ndani ya muda mfupi na kuleta kero kwa Wananchi.

*Katika Kongamano hilo Wananchi wamepata nafasi ya kuelezea kero za Barabara katika maeneo yao na kupatiwa majibu na Wataalamu wa Barabara ambapo wapo waliochangia kwa njia ya Simu huku Simu nyingine zikitokea Mikoani.

*Amesema* huu ni mwisho wa Barabara za mashimo kuonekana kwenye Mkoa wake kwakuwa amejipanga kuhakikisha Barabara zote zinazotengenezwa zinakuwa zenye ubora wa hali ya juu.

*Makonda* amewaagiza Wakuu wa Wilaya zote kuhakikisha wanasimamia ipasavyo ujenzi wa Barabara zinazojengwa katika bajeti iliyotengwa kwaajili ya barabara katika mwaka wa fedha *2017- 2018* ili kuhakikisha Barabara zinakuwa za viwango.

Aidha *Makonda* ameagiza *DAWASCO* kuhakikishe wanapatia ufumbuzi tatizo la utiririshaji wa Maji kwenye Barabara na makazi ya watu kutokana na uchakavu wa Miundombinu unaochangia pia upotevu wa Maji.

*Amesema* Sekta ya Barabara ndio kichocheo kikubwa cha Biashara na Uchumi wa Taifa hivyo lazima Barabara za jiji la Dar es salaam ziwe na kiwango ili kufikia azma ya *Rais Dr. Magufuli* kutaka jiji hilo kuwa la kibiashara.

Amesema Wageni wengi wakiingia Nchini wao hushukia Dar es salaam hivyo jiji hilo kuendelea kuwa na Barabara mbovu ni taswira mbaya kwa Nchi.

Mbali na hayo *Makonda* ametoa siku 30 kwa Wakandarasi walioweka vifusi Barabarani kuhakikisha wanavisambaza sababu vimekuwa kero kwa watumiaji wa Barabara.

*RC Makonda* pia ameagiza *TANROAD* kuhakikisha Taa za Barabarani katika maeneo mbalinbali zinawaka ili kupunguza uharifu.

Hata hivyo amemuagiza Mkuu wa Wilaya ya Ilala Sophia Mjema kuhakikisha Wahandisi wote wa Barabara Manispaa hiyo ambao wamegoma kuhudhuria Kongamano la leo kufika Ofisini kwake siku ya jumatatu wakiwa na maelezo yakutosha.

Katika uchunguzi aliofanya Makonda amebaini ya kuwa makampuni mengi ya ujenzi yanaazima vifaa kwenye makampuni mengine ili waweze kupatiwa ujasili na pindi wanapopewa tenda ya ujenzi hujikuta wanakosa vifaa na wataalam hali inayopelekea kufanya kazi chini ya kiwango pia kuchelewa kukamilika kwa kazi.

Katika hatua nyingine Makonda amemuagiza Katibu Tawala Mkoa kuhakikisha hakuna mtumishi yoyote amesafiri kikazi nje ya Mkoa bila kutoa taafifa kwake baada ya kubaini uwepo  wa Watendaji wanaojipangia safari za kikazi nje ya Mkoa.

Tayari miradi mbalimbali ya ujenzi wa barabara inaendelea katika maeneo mbalimbali ya jiji hilo ambako iko miradi inayotekelezwa na TANROAD, Manispaa na TARURA ambako kukamilika kwakeitasaidia kupunguza adaha kwa wananchi.




TAZAMA LIVE ALICHOKIONGEA MAKONDA KUHUSU DAR YETU


No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages