A great place to access the latest news and information.

Breaking

Post Top Ad

Your Ad Spot

Wednesday, August 9, 2017

RC MAKONDA ATOA SIKU 3 KWA MHANDISI WA UMEME MANISPAA YA KINONDONI KUTENGENEZA MCHORO WA UMEME WA SOKO LA BUJU B.


Mkuu wa mkoa wa Dar es salaam, Paul Makonda ametoa siku tatu kwa mhandisiwa wa umeme wa Manispaa ya Kinondoni kuwasilisha mchoro wa miundombinu ya umeme ya soko la Bunju B ili  Tanesco iweze kuunganisha umeme katika soko hilo.

Mhe. Makonda  ametoa agizo hilo alipo kuwa akisikiliza kero za wananchi katika viwanja vya soko hilo baada ya kuelezwa na mhandisi wa Tanesco mkoa wa  Tanesco  Kinondoni kuwa manispaa waliagizwa kupeleka  mchoro tangu mwezi April mwaka huu lakini hadi leo hawajafanya hivyo, jambo ambalo limesababisha usumbufu mkubwa kwa wafanya biashara wanaofanya biashara sokoni hapo.

Aidha Rc Makonda ameagiza viwanjavyote ambavyo viko wazi havija jengwa vinavyo zunguka soko hilo virudishwe katika miliki ya soko hilo kwakuwa eneo kubwa la soko hilo limeuzwa bila utaratibu ambapo hapo awali lilikuwa hekali 9 na sasa limebakia ekali mbili pekee, awali kabala ya kutoa maamuzi hayo wananchi walilalamika kuhusu ardhi hiyo na kuonyesha kutokuwa na imani na ungozi wa soko hilo na kuwatuhumu kuuza ardhi kinyemale.

Pamoja na hayo Rc Makonda amewataka watumishi na watendaji serikali mkoani humo kufanya kazi kwa bidii na kushughulikia kero na changamoto za wananchi ilikuweza kuleta maendeleo na kutekeleza ilani ya CCM.

“watendaji tuna mchosha Rais kwa mambo madogomadogo ambayo tungeweza kuyamaliza sisi huku chini yeye tuka mwacha akashughulikia mabo makubwa ,huyo huyo ashughulikie makinika , Mafisadi , Bomba la Mafuta halafu sisi tuwe tumekaatu haiwezekani lazima tuwajibike “alisema Makonda
Kwa upande wao wanachi hao wakizungumza ma mhe. Makonda katika mkutano wa hadhara wamesema kuwa tatizo kubwa linalo kabili sokohilo ni ukosefu wa umeme,Maji ya kutosha, uchache wa matundu ya choo  na kero ya baadhi ya wafanya biashara kukimbilia kwenda kufanya kazi barabarani.
Wanachi hao wameomba soko hilo kufanywa sehemu muhimu ya ya kuuza mazao na bidha kwa jumla ili kupunguza msongamano katika masoko mengine,na kulifanya soko hilo kuwa enemuhimu la kibiashara pia itasaidia kuwatoa wote wanaofanya biashara katika maeneo ya pembezoni mwa barabara.

Aidha wananchi hao wameeleza kero ya kupasuka kwa mabomba ya maji (DAWASCO) ambapo Mhandisi wa Dawasco Bw. Aron Joseph ambapo amesema kuwa hali hiyo ya kupasuka ni inatokana na masuala ya kiufundi ambapo kumekuwa na presha (Msukumo) kubwa wa maji kutokana na ukosefu wa matanki ya kutosha.

Hata hivyo Mhandisi Aron ametoa siku mbili kwa Meneja Mkoa bagamoyo Meneja wa DAWASCO kanda ya Tegeta na Bagamoyo Edga Zawa pamoja na Meneja Mkoa Tegeta Ambokile kuhakikisha mabomba yote yanayomwaga maji yanazibwa haraka ili kuondoa keo kwa wananchi hao.

Ziara hiyo ya Mkuu wa mkoa imekuja mara baada ya wanachi wa eneo hilo kusimamisha msafara wa Rais Magufuli alipokuwa njia kurejea Dar es salaam akitokea Tanga na kumweleza kero zinazowakabili hasa kutokana na soko la Bunju B.

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages