Mkuu
wa Mkoa wa Singida Dkt Rehema Nchimbi akionja asali katika moja ya
mabanda ya maonyesho ya nanenane kanda ya kati yanayofanyika katika
viwanja vya Nzuguni, Manispaa ya Dodoma.
Mkuu
wa Mkoa wa Singida Dkt Rehema Nchimbi akitazama bidhaa za mbogamboga
katika banda la Wilaya ya Kondoa katika maonyesho ya nanenane kanda ya
kati yanayofanyika katika viwanja vya Nzuguni, Manispaa ya Dodoma.
Mkuu
wa Mkoa wa Singida Dkt Rehema Nchimbi akisaini kitabu cha wageni katika
banda la Mkoa wa Singida katika maonyesho ya nanenane kanda ya kati
yanayofanyika katika viwanja vya Nzuguni, Manispaa ya Dodoma.
Mkuu
wa Mkoa wa Singida Dkt Rehema Nchimbi akionyeshwa shamba la mahindi
lilostawi vizuri katika maonyesho ya nanenane kanda ya kati
yanayofanyika katika viwanja vya Nzuguni, Manispaa ya Dodoma.
Mkuu
wa Mkoa wa Singida Dkt Rehema Nchimbi akipokea zawadi ya kikapu kutoka
kwa Mkuu wa Jeshi la Magereza Mkoa wa Dodoma SACP Julius Sang’udi
alipotembea banda la jeshi la magereza kujionea bidhaa wanazotengeza
katika maonyesho ya nanenane kanda ya kati yanayofanyika katika viwanja
vya Nzuguni, Manispaa ya Dodoma.
Mkuu
wa Mkoa wa Singida Dkt Rehema Nchimbi akitoka katika banda la Tume ya
taifa ya Umwagiliaji, kushoto kwake ni Mkuu wa Wilaya ya Ikungi Miraji
Mtaturu katika maonyesho ya nanenane kanda ya kati yanayofanyika katika
viwanja vya Nzuguni, Manispaa ya Dodoma.
Maonyesho
ya nane nane yanatakiwa kuweka alama chanya na kuwa na sura ya
mabadiliko yanayoonekana kwa macho kwa wakulima na wafugaji wanaoshiriki
pamoja na wananchi wanaopata huduma na bidhaa katika maonyesho hayo.
Mgeni
rasmi katika Ufunguzi wa maadhimisho ya nanenane kanda ya kati ambaye ni
Mkuu wa Mkoa wa Singida Dkt. Rehema Chimbi ametoa rai hiyo mapema jana
kwa wakulima, wafugaji na washiriki wakati akifungua rasmi maonyesho
hayo huku akiwataka washiriki hao kuitumia fursa hiyo kwa manufaa zaidi.
“Ni
vizuri maadhimisho ya Mwaka huu yakaonesha mabadiliko chanya kwa
washiriki mliojitokeza katika kuonesha bidhaa zenu mbalimbali na pia kwa
wale wote waliofika kwaajili ya kununua au kupata maelezo ya matumizi
ya bidhaa hizo, wapate kitu tofauti kitakachooneka katika maisha yao”,
amesema.
Dkt
Rehema Nchimbi ambaye ametumia muda usipungua dakika 45 kusisitiza
umuhimu wa kuwekeza katika kilimo na ufugaji wenye tija ili kuendana na
falsafa ya serikali ya awamu ya Tano inayo himiza zaidi Uchumi wa
Viwanda.
Aidha
ameliomba Jeshi la Magereza na wawekezaji wote wa ndani na nje ya Nchi
wafike kuwekeza katika mikoa ya Singida na Dodoma na kwa kushirikiana na
Mkuu wa Mkoa wa Dodoma watahakikisha wanatengeneza mazingira rafiki kwa
kila atakayekuwa tayari kuwekeza katika Mikoa hiyo.
“Nimepita
kwenye banda la Jeshi la Magereza na kuona bidhaa nyingi sana
zilizotengenezwa na Ngozi na wamenihakikishia kuwa kiwanda chao kina
uwezo wa kununua ngozi yote inayopatikana katika Mikoa ya Singida na
Dodoma hivyo ni vizuri tutumie hiyo kama fursa” ameongeza Dkt Nchimbi.
Dkt
Nchimbi amesisitiza kuwa Mikoa ya Singida na Dodoma haina ukame na ndio
maana hivi sasa ameanzisha mpango maalum wa kilimo cha umwagiliaji
kwakuwa watafiti wamewahakikishia kuwa mikoa hiyo ina kiwango kikubwa
cha maji ardhini huku yakiwa karibu na uso wa ardhi.
Pia
amewataka wananchi wa Mikoa ya Singida na Dodoma kuacha kabisa kukata
miti kwa kisingizio cha kujikwamua kiuchumi kwasababu kuna njia nyingi
sana za kuondokana na hilo badala ya kuharibu misitu.
“Kule
Singida nimeanzisha kampeni inayojulikana kama ‘ACHIA SHOKA, KAMATA
MZINGA’ ambayo inampa mwananchi nafasi ya kuamua kuacha kukata mti na
badala yake anafuga nyuki jambo linalomsaidia kujikwamua kiuchumi kwa
muda mrefu zaidi kwasababu unaweza kuukata mara moja tu lakini mzinga
unaweza kuutundika mara nyingi kadri uwezavyo”.
Dkt.
Nchimbi alimalizia hotuba yake kwa kuwasisitiza maafisa kilimo kupeleka
kalenda za kilimo katika ngazi zote kuanzia ngazi ya kijiji ili iwe
rahisi kwa Mkulima kujua aina ya mazao anayoweza kulima kwa Mwaka husika
badala ya kumsubiri Mkulima apate madhara kwanza ndipo aje apewe elimu
ya mazao aliyotakiwa kulima kwa mwaka husika.
Maadhimisho
ya 21 ya Sikukuu ya Wakulima na Wafugaji maarufu kama NANENANE
yamefunguliwa rasmi tarehe 3 Agost 2017 kwa kanda ya kati inayojumuisha
mikoa ya Singida na Dodoma.
No comments:
Post a Comment