TAASISI
ya Tafiti za Kiuchumi na Kijamii (ESRF) imefanya mhadhara mkubwa
ulioshirikisha wanazuoni mbalimbali kujadili historia na nafasi ya
kilimo na sera zake katika kufanikisha safari ya viwanda ya Tanzania,
kwa kuangalia mazao ya chakula kama mazao ya biashara.
Katika
mhadhara huo msemaji Mkuu alikuwa Prof. Brian Van Arkadie, majadiliano
yalitanguliwa Prof Samuel Wangwe na Aloyce Hepelwa Akiwasilisha mada
yake aliwataka wataalamu kubadilika katika namna ya kusaidia kuongeza
tija katika kilimo na kuachana na dhana za zamani kwamba wakulima
wameshindwa kubadilika na kukwamisha maendeleo.
Amesema
katika mjadala huo wa hadhara kuhusu maendeleo ya kilimo kutoka wakati
wa uhuru hadi sasa katika jengo la mikutano la ESRF mjini hapa alisema
kwamba tafiti nyingi zimekuwa zikishutumu wakulima kwa kuwa na muono
mdogo na kubisha mabadiliko yanayohitaji kuongeza uzalishaji.
Mkurugenzi
Mtendaji wa Taasisi ya Tafiti za Kiuchumi na Kijamii (ESRF), Dk. Tausi
Kida akitoa neno la ukaribisho kwa washiriki wa mhadhara mkubwa
ulioshirikisha wanazuoni mbalimbali kujadili historia na nafasi ya
kilimo na sera zake katika kufanikisha safari ya viwanda ya Tanzania,
kwa kuangalia mazao ya chakula kama mazao ya biashara uliofanyika katika
ukumbi wa mikutano wa ESRF jijini Dar es Salaam.
Aidha
alisema kwamba kumekuwepo na tafiti zinazoonesha kwamba kilimo
kimekwama katika uasili wake na kuhitajika tafiti za kuona namna bora ya
kukikwamua. Hata hivyo alisema profesa huyo, kumekuwepo na mabadiliko
ya maana katika uchumi wa vijijini, hasa kwa kuangalia uhalisia wa
uchumi kwa kuzingatia fursa za kiuchumi na masoko katika maisha ya
wanakijiji.
Alisema
kutokana na mabadiliko hayo ni dhahiri kusema kwamba wakulima
hawabadiliki ni kushindwa kwa wataalamu ambao ndio walibuni na kupanga
mipango ambayo haikuweza kuwanufaisha wakulima. Profesa Brian Van
Arkadie ambaye pia alishawahi kuwa Mhadhiri Chuo Kikuu cha Dar es salaam
na miongoni mwa watafiti ESRF anasema kuna hatua mbalimbali
zilizofikiwa na wakulima wa Tanzania tangu uhuru na kwamba kuna uhusiano
kati ya kilimo na maendeleo yaliyopo sasa.
Alisema
katika mkutano huo wa hadhara ulilenga kuchambua masuala muhimu
yanayojitokeza katika kilimo cha Tanzania na kuona namna bora ya
kukabiliana na changamoto hizo kwa maendeleo ya taifa, kuwa kuanzia
miaka ya 1970 mazao kwa ajili ya masoko ya nje yaliporomoka sana na
kusababisha taifa kutafuta njia nyingine ya kurekebisha hali hiyo
ikiwamo kuanzishwa kwa mradi wa kubadili kilimo wa SAGCOT.
Prof.
Brain Van Arkadie ambaye ni msemaji mkuu wa mhadhara mkubwa
ulishirikisha wanazuoni mbalimbali kujadili historia na nafasi ya kilimo
na sera zake katika kufanikisha safari ya viwanda ya Tanzania, kwa
kuangalia mazao ya chakula kama mazao ya biashara akiwasilisha utafiti
wake katika mkutano huo ulioandaliwa na ESRF na kufanyika jijini Dar es
Salaam.
Ingawa
mazao hayo ya kilimo yameonakana kuporomoka kutoka miaka hiyo,
kumekuwepo na ongezeko kubwa la pengo la kipato kati ya watu wa mijini
na vijijini huku ukuaji wa vijijini ukikumbwa na udumavu. Pamoja na
ukweli huo amesema profesa huyo, kuna mabadiliko ya kutosha katika
maeneo ya vijijini na katika kilimo kwamba kusema hakuna maendeleo si
kitu sahihi.
Alisema
zipo sababu za kupungua kwa uzalishaji wa mazao makuu kama kahawa,
tumbaku, mkonge na hilo linatokana na serikali kuingilia kati mfumo wa
masoko ambao haukuwa unaswihi. Profesa huyo alisema hata hivyo, kwa
miaka 50 kilimo cha Tanzania kimefanikiwa kulisha taifa kwa kuwezesha
watu wa mijini na vijijini kupata vyakula hasa vile vya msingi ingawa
wakati mwingine ukame ulileta usumbufu.
Huku
Tanzania ikiwa na ongezeko la watu kutoka milioni 12.3 kwa mwaka 1967
hadi milioni 44.9 kwa mwaka 2012 ni dhahiri ukuaji wa kilimo umesaidia
kuiweka nchi katika hali bora zaidi ya upatikanaji wa chakula ingawa
ifikapo mwaka 2030 watu wa mijini watakuwa wameongezeka kwa asilimia 37
na kuweka shinikizo ambalo kwa namna nyingine linaweza kuwa na maana kwa
kuwa mazao ya chakula yatakuwa ndiyo ya biashara na hivyo kuacha
kutegemea yale ya asili kama kahawa na tumbaku.
Mtafiti
mshiriki mwandamizi wa ESRF Prof Samuel Wangwe akijadili mada
iliyowasilishwa na Prof Brian Van wakati wa mhadhara mkubwa
ulioshirikisha wanazuoni mbalimbali kujadili historia na nafasi ya
kilimo na sera zake katika kufanikisha safari ya viwanda ya Tanzania,
kwa kuangalia mazao ya chakula kama mazao ya biashara uliofanyika katika
ukumbi wa mikutano wa ESRF jijini Dar es Salaam.
Katika
utafiti mwaka 2007, imeonekana kwamba nusu ya mapato ya watu wa Dar es
salaam yamekuwa yakitumika kwa ajili ya kununua chakula na kufanya kiasi
kikubwa cha kazi za kilimo katika mazao ya chakula kuwa biashara nzuri
kwa wakulima.Katika mada yake profesa huyo alisititiza kwamba hakuna
shaka maendeleo nchini katika kilimo yapo lakini tafiti nyingi
zimeshindwa kuelekeza kisahihi maendeleo hayo na ukweli wa kutoneemeka
kwa wakulima.
Akijadili
mada hiyo ya Prof. Brian Van Arkadie, Mtafiti mshiriki mwandamizi wa
ESRF Prof Samuel Wangwe ameshauri serikali kutonakili mikakati na sera
za nchi zilizoendelea wakati wa utekelezaji wa mikakati ya kugeuza nchi
kuwa taifa la uchumi wa kati linalotegemea viwanda. Alisema hayo katika
mhadhara kuhusu kilimo nchini kwamba si sawa kunakili sera na mikakati
ya nchi zilizoendelea kama Uingereza, Asia ama Marekani katika
kutekeleza sera ya viwanda bali ibuni yenyewe kwa kuzingatia hali
iliyopo.
Mhadhiri
mwandamizi kitengo cha kilimo uchumi katika Chuo Kikuu cha Dar es
Salaam, Prof Aloyce Hepelwa akijadili mada iliyowasilishwa na Prof Brian
Van wakati wa mhadhara mkubwa ulioshirikisha wanazuoni mbalimbali
kujadili historia na nafasi ya kilimo na sera zake katika kufanikisha
safari ya viwanda ya Tanzania, kwa kuangalia mazao ya chakula kama mazao
ya biashara uliofanyika katika ukumbi wa mikutano wa ESRF jijini Dar es
Salaam.
Akizungumza
wakati akijadili mada iliyowasilishwa na Prof Brian Van Arkadie kutoka
Uingereza kuhusu mazao ya chakula kama ndio mazao ya biashara katika
mikakati ya muda mrefu ya kubadili kilimo cha Tanzania na athari za
kisera, Prof Samuel Wangwe alisema kila nchi ina njia yake ya kufikia
ustawi na neema ya viwanda na hivyo Tanzania lazima ifuate njia yake na
sio kunakili. “Hatuwezi kupita njia ambayo nchi kama Uingereza, Japan,
au nchi za Ulaya zimepita wakati wakikua kiviwanda, lakini tuwe na njia
yetu katika kuelekea uchumi wa viwanda .
Kama
hatutakuwa makini hatutafanikiwa,” alisema. Prof Wangwe pia alisema
kwamba mapinduzi ya Kilimo lazima yapewe kipaumbele kama taifa linataka
kuwa na uchumi wa viwanda. Akikaribisha wadau kushiriki katika mhadhara
huo Mkurugenzi Mtendaji wa ESRF, Dk. Tausi Kida alisema kwamba mhadhara
huo ulikuwa ni njia muafaka ya kubadilisha maarifa ili kuboresha kilimo
cha Tanzania kwa kukipatia kilimo hicho mkakati wa muda mrefu wa
kubadilika.
Picha
juu na chini ni baadhi ya wageni waalikwa wanazuoni mbalimbali
wakiwasilisha maoni yao wakati wa mhadhara wa kujadili historia na
nafasi ya kilimo na sera zake katika kufanikisha safari ya viwanda ya
Tanzania, kwa kuangalia mazao ya chakula kama mazao ya biashara
uliondaliwa na ESRF na kufanyika jijini Dar es Salaam.
Alisema
katika kuimarisha kilimo hicho ni vyema masuala yanayogusa mazao ya
chakula na yale ya kupeleka nje na sera kuangaliwa kwani masuala hayo
yana athari za muda mrefu katika ukuaji wa kilimo. Katika hadhira hiyo
aliwataka washiriki kuangalia kwa makini historia ya kilimo nchini, sera
na kuona athari za muda mrefu na fupi za sera zilizopo na kama kweli
wataalamu wametekeleza wajibu wao katika kutafuta suluhu ya wakulima au
kuendelea kudai kwamba wakulima hawako tayari kubadilika.
Dk.
Kida alisema kwa kuangalia historia ya kilimo Tanzania wataalamu hao
watakuwa na nafasi kubwa ya kuchangia katika kuendeleza kilimo ambacho
ni msingi mkubwa wa maendeleo ya mtu mmoja mmoja, kwani wapo asilimia 80
wakitegemea kilimo na taifa ambalo linataka kwenda katika uchumi wa
viwanda ambavyo mali ghafi zinategemewa kutoka katika sekta ya kilimo.
Aidha
alimshukuru Prof. Brain Van Arkadie ambaye ndiye alikuwa msemaji mkuu
kwa utafiti alioufanya ambao aliuwasilisha mbele ya mkutano wa wasomi
mbalimbali. Prof. Van Arkadie ambaye ni veteran ambaye alishawahi
kushiriki katika mpango wa miaka mitano wa kwanza wa maendeleo mwaka
1963. Na kufanyakazi katika maeneo mbalimbali katika nchi za Afrika
Mashariki na Chuo Kikuu cha Dar es salaam.
Mwenyekiti
wa mhadhara huo Profesa wa Kilimo Uchumi kitengo cha Uchumi katika Chuo
Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM), Lucian Msambichaka akiendesha mhadhara
huo. Kulia ni Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Tafiti za Kiuchumi na
Kijamii (ESRF), Dk. Tausi Kida na kushoto ni Prof. Brain Van Arkadie
ambaye ni msemaji mkuu wa mhadhara huo.
Prof. Brain Van Arkadie ambaye ni msemaji mkuu wa mhadhara huo akifafanua jambo wakati wa kipindi cha maswali na majibu.
Pichani
juu na chini ni sehemu ya wanazuoni na wadau kutoka taasisi mbalimbali
walioshiriki kujadili historia na nafasi ya kilimo na sera zake katika
kufanikisha safari ya viwanda ya Tanzania, kwa kuangalia mazao ya
chakula kama mazao ya biashara katika mhadhara huo ulioandaliwa na ESRF
na kufanyika jijini Dar es Salaam.


Picha
ya pamoja ya washiriki wa mhadhara mkubwa ulioshirikisha wanazuoni
mbalimbali kujadili historia na nafasi ya kilimo na sera zake katika
kufanikisha safari ya viwanda ya Tanzania, kwa kuangalia mazao ya
chakula kama mazao ya biashara ambao uliandaliwa na ESRF na kufanyika
jijini Dar es Salaam
Mkurugenzi
Mtendaji wa Taasisi ya Tafiti za Kiuchumi na Kijamii (ESRF), Dk. Tausi
Kida akibadilishana mawazo na wageni waalikwa baada ya kumalizika kwa
mhadhara huo ulioandaliwa na ESRF na kufanyika jijini Dar es Salaam
No comments:
Post a Comment