A great place to access the latest news and information.

Breaking

Post Top Ad

Your Ad Spot

Thursday, August 3, 2017

BENKI YA FINCA MICROFINANCE YAZINDUA KAMPENI YA FikaNaFINCA

Meneja wa Masoko wa Benki ya Finca Microfinance Bw. Nicholous John, akionyesha mfano wa tiketi ya ndege itakayotumika katika kampeni yao iliyopewa jina la FikaNaFINCA iliyozinduliwa jana jijini Dar es Salaam. Pembeni yake ni Afisa Mawasiliano wa Shirika la ndege la Tanzania ATCL Bi. Lilian Fungamtama.
Kutoka kushoto ni Meneja usafirishaji wa kampuni ya Super Feo Bw. Masumbuko akifuatiwa na Meneja wa Masoko wa Benki ya Finca Microfinance Bw. Nicholous John, Afisa Mawasiliano wa Shirika la ndege la Tanzania ATCL Bi. Lilian Fungamtama na Mtaalam wa Masoko wa Benki ya FINCA Bw. Noel Mulumba wakionyesha mifano ya tiketi za usafirishaji ambazo wateja watapaswa kupiga picha na kushirikisha wafuasi wako katika mitandao ya kijamii ili kujishindia tiketi ya bure katika kampeni iliyopewa jina la FikanaFINCA.

Dar es Salaam, Agosti 2, 2017 - Moja ya Benki inayokua kwa kasi nchini, Benki ya FINCA Microfinance, leo imetangaza kampeni ya miezi miwili inayofahamika kama 'FikaNaFINCA' Kampeni hii itampa fursa anayefwatilia kurasa za kijamii ya benki hiyo nafasi ya kujishindia tiketi ya kwenda na kurudi bure baada ya kuposti picha ya bahasha ya tiketi yenye nembo ya FIKA NA FINCA na pia kupendwa na watu wengi.

Akizungumza katika mkutano wa waandishi wa habari katika makao makuu ya benki jijini Dar es Salaam, Meneja wa Masoko wa Benki ya Finca Microfinance, Nicholus John alisema kuwa washindi watakuwa na nafasi ya kupata tiketi za usafiri wa anga na barabara ya kwenda na kurudi kutoka mashirika ya usafiri wa anga ya ndani ya Air Tanzania (ATCL) na Auric Air na pia kwa mabasi yanayoenda bara yakiwemo mabasi ya kampuni za Ngorika, New Force na Isamilo.

"FINCA inathamini wateja wake na jamii kwa ujumla, katika kuonyesha hilo, ndo maana tumeleta kampeni hii itakayoenda kwa miezi miwili huku mshindi kutangazwa kila wiki. Jinsi ya kushinda ni rahisi sana, piga picha tiketi yako yenye nembo ya FIKA NA FINCA, posti kwenye kurasa ya Facebook na Instagram ukiweka #FikaNaFINCA kwenye caption, alafu aalike ndugu jamaa na marafiki kuipenda."alisema John.

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages