Baba Mzazi wa Msanii Diamond Platinum, Abdul Naseeb amefunguka kuhusu tetesi zinazoendelea za mtoto wake kutajwa kuwa ndiye mzazi halali wa mtoto wa mlimbwende Hamisa Mobeto anayetambulika kwa jina la Abdul Naseeb ambalo ndiyo jina la baba yake na Diamond.
Akizungumza katika kipindi cha SHILAWADU cha Clouds TV Ijumaa hii, Baba Diamond ameeleza kuwa kama Diamond ameamua kumpa mtoto huyo jina lake ni upendo na inaonesha thamani kwake.
Baba Diamond amesema hawezi kumlaumu mwanaye Diamond kwa kilichotokea kwani yeye ni msanii mkubwa anakumbana na vishawishi mbalimbali, hivyo cha kufanya asiendekeze zinaa awaoe wanawake aliozaa nao (Hamisa Mobeto na Zarina Hassan) na awatendee haki kwa kutoa huduma sawa.
Kuhusu wajuukuu zake, Mzee Abdul ameeleza kuwa yeye anawapenda wote ingawa hajawahi kumuona hata mmoja.
Alhamisi hii Diamond aliandika maneno makali mtandaoni yaliyohusishwa kwenda Mobetto ambaye siku chache zilizopita alitangaza jina mwanaye kuwa Abdul Naseeb. Hatua hiyo iliwafanya mashabiki wengi ambao walitaka kumjua baba wa mtoto huyo wa Mobetto kuwa ni Diamond.
Hata hivyo mpaka sasa mkali huyo wa wimbo Eneka hajawahi kutoa neno lolote juu ya mtoto huyo licha ya mama yake pamoja na dada yake Esma kuonekana mara kadhaa wakimtembelea mrembo huyo wakati alipojifungua katika hospitali moja jijiji Dar es salaam.
No comments:
Post a Comment