Katika
kuhakikisha dhamira ya Serikali ya dhamira ya Serikali ya kujenga
Uchumi wa Viwanda wadau wa kilimo na viwanda wamekutana ili kuzungumzia
nafasi ya Benki ya Maendeleo ya Kilimo ya Tanzania (TADB) katika
kuhakikisha Benki hiyo inasaidia sekta ya Kilimo nchini.
Wakizungumza
katika Kikao hicho kilichoandaliwa na TADB ili kujadili mikakati ya
kuboresha uwezeshaji kwenye kilimo na viwanda nchini.
Akizungumza
katika kikao hicho Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa TADB, Bw. Francis
Assenga amesema kuwa Benki imejipanga kuleta matokeo makubwa kwenye
mapinduzi ya kilimo na viwanda hasa vya uchakakataji na usindikaji wa
mazao ya kilimo.
Bw.
Assenga amesema kuwa mipango hii itasaidia upatikanaji wa mali ghafi
kwa viwanda vya ndani hivyo kusukuma ndoto ya Serikali kufikia lengo
lake la Kujenga Uchumi wa Viwanda na kuhuisha uwekezaji kwenye Viwanda
vidogo vidogo na vya kati vya usindikaji na uchakataji wa mazao ya
Kilimo na mifugo.
“Benki
imejikita kwenye kusaidia Sekta ya Kilimo iweze kusukuma dhamira ya
Serikali ya Uchumi wa Viwanda uweze kutoa matunda yaliyokusudiwa ili
kuchagiza na kusaidia Mapinduzi ya Kilimo kutoka kilimo cha kujikimu
kwenda cha kibiashara ili kuchangia kwenye ukuaji wa uchumi na kupunguza
umaskini,” alisema.
Bw.
Assenga amesema katika kuhakikisha azma hiyo inatimia TADB imejipanga
kutoa elimu ili kuwajengea uwezowakulima na taasisi mbali mbali za fedha
pamoja na vyama vya ushirika kuweza kukopa toka TADB pamoja na
kushirikiana na wadau mbali mbali kusaidia uwekezaji mkubwa kwenye Sekta
ya Kilimo ili iweze kuinua pato la Taifa na kumkomboa Mwananchi.
Kaimu
Mkurugenzi Mtendaji huyo ameongeza kuwa TADB imeanza kujiimarisha na
kuchochea mabenki na taasisisi za fedha kuongeza utoaji wa mikopo na
fedha zingine kwenye Sekta ya Kilimo ili kuongoza utoaji mikopo ya
uongezaji wa thamani katika shughuli za kilimo.
TADB
ni taasisi ya serikali ambayo ilianzishwa kwa ajili ya kutatua ufinyu
mkubwa wa upatikanaji wa fedha mikopo kwa ajili ya maendeleo ya kilimo
nchini ambao ulikuwa unachangiwa kwa kiasi kikubwa na mikopo mingi
kutoka taasisi za fedha kuelekezwa zaidi kwenye upande wa biashara za
bidhaa; riba kubwa kwenye mikopo ya kilimo; mikopo ya muda mfupi;
masharti magumu ya kukopa bila kuzingatia hali halisi ya sekta ya kilimo
na mazao ambayo inaathiriwa kwa kiasi kikubwa na mabadiliko ya hali ya
hewa.
Mwenyekiti
wa Bodi ya Wakurugenzi ya Benki ya Maendeleo ya Kilimo ya Tanzania
(TADB), Bibi Rosebud Kurwijila (kushoto) akizungumza na aliyewahi kuwa
Katibu Mkuu wa Wizara ya Kilimo, Mzee Peniel Lyimo (kulia) wakati wa
Kikao cha Wadau wa Kilimo Kujadili Mikakati Ya Kuboresha Uwezeshaji
Kwenye Kilimo Na Viwanda kinachofanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa
Kimataifa wa Julius Nyerere (JNICC) Dar es Salaam.
Mwenyekiti
wa Kamati ya Biashara ya TADB, Bibi Rehema Twalib (kulia) akizungumza
wakati wa Kikao cha Wadau wa Kilimo Kujadili Mikakati Ya Kuboresha
Uwezeshaji Kwenye Kilimo Na Viwanda kinachofanyika katika Ukumbi wa
Mikutano wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNICC) Dar es Salaam.
Aliyewahi kuwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Kilimo, Mzee Peniel Lyimo (kulia) akiongoza Kikao hicho.
Kaimu
Mkurugenzi Mtendaji wa TADB, Bw. Francis Assenga (kushoto) akisisitiza
nafasi ya Benki yake katika kuleta matokeo makubwa kwenye mapinduzi ya
kilimo na viwanda hasa vya uchakakataji na usindikaji wa mazao ya
kilimo.
Wajumbe
wa Bodi ya Wakurugenzi wa TADB wakiongozwa na Mwenyekiti wa Bodi, Bibi
Rosebud Kurwijila (kushoto) wakifuatilia kwa makini Kikao hicho.
Washiriki
wa Kikao hicho wakifuatilia mawasilisho mbali mbali wakati wa Kikao cha
wadau wa kilimo waliokutana kujadili mikakati ya kuboresha uwezeshaji
kwenye kilimo na viwanda. Kikao hicho kiliandaliwa na Benki ya Maendeleo
ya Kilimo ya Tanzania (TADB).
Wadau wa kilimo waliokutana kujadili mikakati ya kuboresha uwezeshaji kwenye kilimo na viwanda wakiwa katika picha ya pamoja.
No comments:
Post a Comment