A great place to access the latest news and information.

Breaking

Post Top Ad

Your Ad Spot

Monday, June 19, 2017

Mshindi wa Kampeni ya Akaunti ya Malengo ya NBC akabidhiwa gari lake

Mkuu wa Idara ya Wateja Binafsi  wa Benki ya NBC, Andrew Lyimo  (katikati), akikabidhi kadi ya gari kwa Rose Richard Getenyi kwa niaba ya mumewe, Lawrence Njozi aliyeshinda zawadi ya gari mpya  aina ya Toyota Double Cabin Pick Up baada ya kushiriki katika kampeni ya akaunti ya Malengo ya benki hiyo. Anayeangalia ni Meneja Kitengo  cha  Bidhaa za Kuwekeza, Dorothea Mabonye. Hafla hiyo ilifanyika jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki.

Mkuu wa Idara ya Wateja Binafsi  wa Benki ya NBC, Andrew Lyimo  (katikati), akikabidhi ufunguo wa  gari mpya  kwa Rose Getenyi kwa niaba ya mumewe, Lawrence Njozi aliyeshinda zawadi ya gari mpya  aina ya Toyota Double Cabin Pick Up baada ya kushiriki katika kampeni ya akaunti ya Malengo ya benki hiyo. Anayeangalia ni Meneja Kitengo cha  Bidhaa za Kuwekeza, Dorothea Mabonye. Hafla hiyo ilifanyika jijini Dar es Salaam.

Rose Gitenyi akifurahia kuwasha gari lao Toyota Double Cabin Pick Up jipya ambalo mumewe alijishindia katika kampeni ya akaunti ya Malengo iliyoendeshwa na  NBC.

Familia ya mteja wa Benki ya NBC Lawrence Njozi aliyeibuka mmoja wa washindi wawili wa kampeni ya Malengo ya benki hiyo na kujishindia gari jipya aina ya Toyota Double Cabin Pick Up wakipozi kwa picha mbele ya gari hilo mara baada ya  Mkuu wa Idara ya Wateja Binafsi wa  NBC, Andrew Lyimo (kulia) kumkabidhi mke wa mshindi huyo, Rose Getenyi (wa tano kushoto), jijini Dar es Salaam  mwishoni mwa wiki.

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages