Mkurugenzi wa Manispaa ya
Kigamboni, Stephen Katemba amesema kiwanda cha Lake Cement kinafuata sheria za
utunzaji wa mazingira kwa wananchi wa Kimbiji.
Katemba amesema hayo wakati alipokwenda kusherekea siku ya wafanyakazi na
kushiriki shughuli mbalimbali za kijamii zinazofanywa na Lake Cement, amesema
kuwa kiwanda kwa kufuata sheria ya mazingira na sheria za wafanyakazi kamwe
migogoro haiwezi kutokea.
Amesema kuwa wafanyakazi lazima wafanye kazi kwa kujituma ili kiwanda kiweze kujiendesha katika kuweza kufikia malengo ya kutimiza kwa wafanyakazi wake.
Katemba amesema wakati kitendo cha Kiwanda kudhamini mashindano mbalimbali katika eneo la kimbiji ni kuonyesha kiwanda kinajua wajibu wake.
Makamu wa Rais wa Lake Cement, Afroz Ansary amesema wanawajibu wa kuwa karibu na jamii ya Kimbiji katika shughuli za kijamii. Mafanikio ya kiwanda yanatokana na jamii inayozunguka kushirikiana katika masuala mbalimbali ya kijamii.
Nae Afisa Utumishi wa Kiwanda hicho, Ahmed Mstapha amesema kuwa kiwanda cha Nyati Cement kinatekeleza majukumu yake kwa jamii inayozunguka kiwanda hicho.
Amesema kuwa wataendelea kuwa karibu na wananchi katika shughuli mbalimbali ambazo zinajitokeza katika eneo la Kimbiji.
Mkurugenzi wa Manispaa ya
Kigamboni, Stephen Katemba akizungumza na wafanyakazi mara baada kutembelea
kiwanda hicho katika siku ya wafanyakazi na kushiriki shughuli mbalimbali
ikwemo ya upandaji jijini Dar es Salaam.
Afisa Utumishi wa Manispaa ya
Kigamboni, Cosmas Hinju akizungumza wakati wa shughuli ya upandaji miti katika
kiwanda cha Lake Cement jijini Dar es Salaam.
Makamu wa Rais wa Lake Cement,
Afroz Ansary akizungumza juu ya udhamini wa shughuli mbalimbali zinazofanywa na
kiwanda hicho.
Meneja Rasilimali Watu wa Lake
Cement, Julieth Domel akizungumza juu jinsi wanavyoshugulika na wafanyakazi wa
kiwanda kwa kufuata sheria za Kazi.
Wananchi wakiangalia fainali ya
Kata ya Kimbiji iliyodhaminiwa na Lake Cement jijini Dar es Salaam.
No comments:
Post a Comment