Wabunge
wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania leo siku ya Jumatatu April 24, 2017
wametembelea Ubalozi wa Tanzania nchini Marekani na kukutana na Balozi wa
Tanzania nchini Marekani na Mexico Mhe. Wilson Masilingi. Katika picha toka
kushoto ni Mkuu wa Utawala na Fedha Ubalozi wa Tanzania nchini Marekani Bi.
Swahiba Mdeme,Mwambata wa Jeshi Ubalozi wa Tanzania na Canada Col. Adolph
Mutta, Mwenyekiti wa kamati ya Bunge ya Bajeti Mhe. Hawa A. Ghasia, Balozi wa
Tanzania nchini Marekani na Mexico Mhe. Wilson Masilingi, Mbunge Mhe. Janeth Z.
Mbene, Mhe. Josephat S. Kandege, Afisa wa Ubalozi Bwn. Dismas Assenga na Afisa
wa Bunge Bwn. Godfrey Godwin. Wabunge hao wa Bunge la Jamhuri ya Muungano
waTanzania walikuja Washington, DC kuhudhuria mikutano ya kipupwe ya Benki ya
Dunia na IMF.
Wabunge
wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania wakiwa katika picha ya pamoja na
Balozi wa Tanzania nchini Marekani na Mexico Mhe. Wilson Masilingi. Katika
picha toka kushoto ni Afisa wa Bunge Bwn. Godfrey Godwin, Mwenyekiti wa kamati
ya Bunge ya Bajeti Mhe. Hawa A. Ghasia, Balozi wa Tanzania nchini Marekani na
Mexico Mhe. Wilson Masilingi, Mbunge Mhe. Janeth Z. Mbene, na Mhe. Josephat S.
Kandege


No comments:
Post a Comment