Timu ya mpira wa wavu
(Volleyball) ya wanawake ya Magereza imetwaa ubingwa wa mchezo huo katika mashindano ya
Muungano yaliyofikia tamati jana katika uwanja wa Taifa wa Ndani
jijini Dar es Salaam.
Timu ya Magereza ya
wanawake licha ya kufungwa mchezo wao wa mwisho dhidi ya Jeshi Stars wanawake
kwa seti 3-2 walifanikiwa kuibuka mabingwa kwa tofauti ya pointi.
Kwa upande wa wanaume,
timu ya mpira wa wavu (Volleyball) Jeshi Stars wamefanikiwa kuibuka mabingwa wa
mashindano ya Muungano baada ya kufanikiwa kuwafunga Magereza kwa ushindi wa
seti 3-1.
Mabingwa hao
wamekabidhiwa zawadi pamoja na kikombe na aliyekuwa mgeni rasmi Katibu wa
Baraza la Michezo Tanzania (BMT) Mohamed Kiganja.
Mchezaji wa timu ya mpira
wa wavu (Volleyball) ya Jeshi Stars, Fordey Edward ameibuka mchezaji bora (MVP)
wa mashindano ya Muungano
yaliyofikia tamati jana.
Fordey ameiwezesha timu
yake ya Jeshi Stars kutwaa taji hilo baada ya kuifunga timu ya Magereza katika
mchezo huo wa fainali. Fordey ambaye ni mkazi wa mkoa wa Tabora pia ni mchezaji
wa timu ya Taifa ya mchezo huo.
Nahodha
wa timu hiyo Averine Albert akikabidhiwa kikombe na Mgeni rasmi Ndg. Ahmed
Kiganja ambaye ni katibu wa Baraza la Michezo la Taifa (BMT).
Nahodha
wa timu hiyo ya Jeshi Stars Abel Masunga akikabidhiwa kombe lao.
No comments:
Post a Comment