Wagonjwa wa corona Tanzania wafikia 284, Waziri Mkuu wa nchi ya Tanzania Kassim Majaliwa ametangaza.
Akihutubia katika tukio la ibada ya kitaifa jijini Dar es Salaam leo Jumatano, Majaliwa amesema kufikia Jumanne Aprili 21 wagonjwa waliothibitika nchini humo ni 284 ambapo kati yao 256 wanaendelea vizuri, saba kwenye uangalizi maalumu, 11 wamepona na 10 wamefariki.
Kufikia Jumatatu Tanzania ilikuwa imethibitisha wagonjwa 254, na hivyo wagonjwa 30 zaidi wameongezeka nchini.
No comments:
Post a Comment