Mkuu
wa Jeshi la Polisi nchini IGP Simon Sirro amewataka Maofisa na Askari
Polisi kote nchini kushiriki michezo ili kujenga Afya,ukakamavu na
urafiki baina ya wenyewe kwa wenyewe na raia.
IGP
Sirro ameyasema hayo jijini Dar Es Salaam wakati hafla fupi ya
kuwapongeza wachezaji wa TAEKWONDO waliofanya vizuri katika michezo ya
Taekwondo Pumsae (kucheza Kata), Taekwondo Gyeokpa ( kuvunja kibao kwa
kuruka Juu) na Taekwondo Gyeorugi (Mapigano) iliyomalizika hivi karibuni
ambapo timu ya Polisi iliibuka na ushindi wa kwanza katika timu 17
zilizoshiriki.
Sirro
alisema Jeshi la Polisi litaendelea kutilia mkazo michezo ya aina
mbalimbali na atahakikisha Askari na Maofisa wanapata fursa ya kushiriki
michezo kwakuwa kwakufanya hivyo kutasaidia pia kulitangaza Jeshi la
Polisi na kujenga mahusiano na jamii."Hakikisheni
hamrudi nyuma,tutawapa sapoti ya kila namna ili tusiwe wasindikizaji
bali tuweze kutoa ushindani na kufanya vyema na ni jambo linalowezekana
kwa kuwa ari na morali ipo"Alisema Sirro.
Kwa
Upande wake Mkuu wa Michezo wa Jeshi la Polisi,Kamishna Msaidizi wa
Polisi ACP Philip Kalangi alisema ushindi wa timu hiyo ni chachu katika
kujiandaa na michezo ya majeshi ya EAPCCO itakayofanyika hapa nchini
mwakani ambapo Tanzania itakuwa mwenyeji.
mashindano
hayo yaliyoandaliwa na ubalozi wa Jamhuri ya korea ukishirikiana na
Chama cha Walimu wa Taekwondo kutoka korea (Korean Taekwondo Masters
Association) ambayo ni mashindano ya Taekwondo ya kitaifa yaliyofanyika
tarehe 21/10/2017 ambayo yalishilikisha vilabu 17 vya Taekwondo kutoka
nchi nzima ambavyo ni Makongo Juu, Kariakoo,Shark TKD,Twiga Triple A,HTC
DSM, KILI, Vingunguti,Arusha Morden,TCC,AICC,UAUT pamoja na vilabu vya
Polisi ambavyo ni DPA, MPA na ZPA.
Mkuu wa Jeshi la Polisi Nchini (IGP) Simon Sirro, akiwa na viongozi wa
Jeshi la Polisi Sambamba na Askari Polisi walioshiriki na kujinyakulia
medali mbalimbali katika mashindano ya mchezo wa Taekwondo iliyo
andaliwa na Ubalozi wa Jamuhuri ya Korea ukishirikiana na Chama cha
walimu wa Taekwondo kutoka Korea. (Korean Taekwondo Masters Association)
Mkuu
wa Jeshi la Polisi Nchini (IGP) Simon Sirro, akiwa na askari wa jeshi
hilo wanaounda timu ya Taekwondo ambao walishiriki na kujinyakulia
medali mbalimbali katika mashindano ya Taekwondo yaliyo andaliwa na
Ubalozi wa Jamuhuri ya Korea ukishirikiana na Chama cha walimu wa
Taekwondo kutoka Korea. (Korean Taekwondo Masters Association)
yaliyoshirikisha vilabu 17 vya Taekwondo kutoka nchi nzima.
Mkuu
wa Jeshi la Polisi Nchini (IGP) Simoni Sirro akimvisha medali askari
Polisi ambaye ni miongoni mwa askari waliojinyakulia medali katika
mashindano taekwondo iliyo andaliwa na Ubalozi wa Jamuhuri ya Korea
ukishirikiana na Chama cha walimu wa Taekwondo kutoka Korea. (Korean
Taekwondo Masters Association). Picha zote na Jeshi la Polisi
No comments:
Post a Comment