Mratibu
wa Shirika la Umoja wa Mataifa la dawa za Kulevya na Uhalifu (UNODC)
Bi. Immaculate Nyoni akimkabidhi boksi lenye vifaa vya kupimia mkojo
watumiaji dawa ya Methadon ambao wanatumia aina nyengine ya dawa
kinyume na taratibu katika hafla iliyofanyika Kliniki Methadone
Kidongochekundu.
Rais
wa watumiaji dawa ya Methadon Zanzibar Hilal Nassor akizungumza na
wandishi wa habari baada ya kukabidhiwa vifaa vya kuwatambua watumiaji
wa tiba ya Methadone na baadae kutumia dawa aina nyengine.
Baadhi
ya watumiaji dawa za Methadone wakisubiri kupatiwa huduma katika
Kliniki yao iliyopo Hospitali ya wagonjwa wa akili Kidongo- Chekundu
Mjini Zanzibar.Picha na Makame Mshenga.
Na Ramadhani Ali – Maelezo .
Wagonjwa
wanaotumia dawa aina ya Methadone kama tiba baada ya kuathirika
kutokana na dawa za kulevya na wanaoutumia aina nyengine ya dawa kwa
njia za siri wamepatiwa muarubaini baada ya kupatikana vifaa maalumu vya
kumgundua mtumiaji kwa kumpima mkojo.
Vifaa
hivyo vinavyojulikana kwa jina la DOAKIT vimetolewa na shirika la Umoja
wa Mataifa la kupambana na madawa ya kulevya na uhalifu (UNODC).Mratibu
wa Mradi wa Taifa wa kupambana na HIV/AIDS kwa wafungwa, Immaculate
Nyoni ambae ni afisa wa UNODC Tanzania amemkabidhi vifaa hivyo Mratibu
wa huduma za ukimwi kwa watu wa makundi maalum Zanzibar Dkt. Shaaban
Hassan katika hafla iliyofanyika Kliniki ya Methadone iliopo ndani ya
hospitali ya wagonjwa wa akili Kidongo- chekundu.
Immaculate
alisema UNODC itaendelea kuunga mkono juhudi zinazochukuliwa na
Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kuwapatia tiba sahihi wagonjwa
walioathirika na dawa za kulevya.Alisema
kwa kuanzia wameleta DOAKIT 1500 ambazo zinaweza kutumika kwa kipindi
cha miezi mitatu kwa mujibu wa idadi ya wagonjwa wanaotumia Methadone
waliosajiliwa katika kliniki hiyo.
Daktari
dhamana wa hospitali ya Kidogochekundu Dkt. Khamis Othman alilishukuru
shirika la UNODC kwa kuwapatia msaada huo ambao kwa kipindi cha mwaka
mmoja walikuwa na upungufu mkubwa na kupelekea baadhi ya wagonjwa
kutumia aina nyengine ya dawa bila kujulikana.
Alisema
kwa mujibu wa taratibu za kutumia tiba ya Methadone mgonjwa hatakiwi
kutumia aina nyengine ya dawa za kulevya na akifanya hivyo hupata
madhara makubwa kwa kuongeza kiwango cha dawa mwilini.
Alisema
DOAKIT ni viifaa vyenye uwezo wa kugundua aina sita ya dawa za kulevya
kwa kuchunguza mkojo wa mtumiaji na vinaweza kutumika katika maeneo
mbali mbali kuwachunguza watumiaji wa dawa hizo.Dkt.
Khamis alieleza kuwa Kliniki ya Methadone ya Kidongochekundu
ilianzishwa mwaka 2015 na imesajili wagonjwa 434 ambao wanapatiwa tiba
kamili na imekuwa mkombozi wa vijana wengi waliokubali kujiunga.
Alisema
kazi ya Methadone ni kusaidia kuondosha hamu ya kutumia Heroine na dawa
nyengine za kulevya hatimae mtumiaji huacha kidogo kidogo kutumia dawa
hizo.Hata
hivyo amekiri kuwa bado wanakabiliwa na changamoto kubwa kwani baadhi
ya wagonjwa wanaotumia Methadone hukosekana baadhi ya siku na wanatumia
dawa nyengine za kulevya kwa siri.
Wagonjwa
wanaotumia Methadone wamekiri kuwa inawasaidia kujitambua na
imewarejesha katika mfumo bora wa maisha na wanaaminika ndani ya jamii
zao.
Amina
Omar mkaazi wa Jangombe, alietumia dawa za kulevya kwa miaka 25,
alisema wakati anatumia dawa hizo alikuwa hajitambui na alidhoofu
kufikia uzito wa chini ya kilo 40 na baada ya kutumia Methadone hivi
sasa uzito wake umefikia kilo 80.
No comments:
Post a Comment